Habari za Punde

Umoja wa Serikali ya Wanafunzi ya Skuli ya Turkish Maarif Yatakiwa Kushirikiana na Kuwa Imara Katika Elimu.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar mhe Simai Mohammed Said wa wa pili kulia, akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo bwana Ali Khamis Juma  wa kwanza kushoto wakikagua samani pamoja na vifaa mbalimbali vya michezo ya watoto kwa Skuli ya Maarif Turkish iliopo Mombasa Mjini Unguja, ikiwa lengo ni kuendelea kutoa elimu bora kwa wanafunzi. samani pamoja na vifaa mbalimbali vya michezo ya watoto kwa Skuli ya Maarif Turkish iliopo Mombasa Mjini Unguja, ikiwa lengo ni kuendelea kutoa elimu bora kwa wanafunzi, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Jumuiya ya Tarkish Foundation ya Uturuki Mr Oguz Yilmaz.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe, Simai Mohammed Said (katikati) akiwa katika ftari ya pamoja iliyoandaliwa na Serikalj ya Umoja wa Wanafunzi wa Skuli ya Tarkish Maarif Zanzibar, iliopo Mombasa mjini Unguja.

na Maulid Yussuf WEMA.


Na Maulid Yussuf WEMA                                                                                                                                                 
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Simai Mohd Said Amewataka Serikali ya Umoja wa Wanafunzi wa Skuli ya Turkish Maarif Zanzibar  iliopo Mombasa Unguja kuendelea kushirikiana na kuwa imara ili kujiletea maendeleo katika Elimu.

Akizungumza wakati wa Futari ya pamoja iliyoandaliwa na Serikali ya umoja wa Wanafunzi wa Skuli hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Skuli yao, mhe Simai amewapongeza kwa juhudi kubwa waliyoamua kufanya Ftari hiyo kwa kuwafutarisha walimu wao jambo ambalo linazidisha upendo kati yao.

Amewataka kuendelea kufanya sadaka hiyo pamoja na kushikamana katika masuala mengine ya kielimu, michezo pamoja na kufanya midahalo mbali mbali na Skuli nyengine ili kuweza kufaidika zaidi katika kukuza elimu.

Aidha ameitaka jamii kuondoa dhana ya kuwa Skuli za binafsi zinajiendesha wenyewe bali zinaendeshwa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu, kutokana na kuwa wao ndio inayotoa vibali na kuwasajili pamoja na kuwafuatilia katika mitaala yao ili kwenda sambamba na elimu inayotolewa nchini.

Aidha ametoa shukurani zake kwa umoja wa Serikali ya Wanafunzi wa Skuli hiyo kwa kuamua kumualika yeye kuwa mgeni rasmi ambapi anaimani kuwa  ni kuendeleza mashirikiano kwa Serikali na Skuli za binafsi kafika kukuza sekta ya Elimu nchini.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar bwana Ali Khamis Juma amesema amewataka Wanafunzi pamoja na mambo mengine kujitahidi kusoma kwa bidii ili nao wawe viongozi wazuri wa baadae.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jumuiya Tarkish Foundation ya Uturuki Mr Oguz Hamza Yilmaz amewashukuru na kuwapongeza Uongozi wa Skuli yao pamoja na Wanafunzi kwa kuandaa futari hiyo ambayo imewakutanisha watu kutoka maeneo mbalimbali.

Nao Viongozi wa Serikali ya umoja wa Wanafunzi wa Skuli ya Turkish Maarif iliopo Mombasa, wamewashukuru Walimu wao kwa kuwaunga mkono kutekeleza futari hiyo pamoja na washiriki wote walidhuria katika futari yao na kuwaomba kuendelea kuwaunga mkono kila watakapowahitaji katika kuleta maendeleo ya Elimu katika Skuli yao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.