Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa akimsikiliza Kada wa CCM, Jamal Tamimu (katikati) alipomuombea kura mgombea wa CCM Dkt Florence Samizi (kulia) katika Uchaguzi Mdogo kwenye Jimbo la Muhambwe Mkoani Kigoma, katika uzinduzi wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa wa Kibondo, Mei 4, 2021. Tamimu alikuwa ni mmoja wa WanaCCM wenye ushawishi mkubwa walioshiriki katika kura za maoni kuwania uteuzi wa Chama chao.
Kada wa CCM, Jamal Tamimu akimuombea kura mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mdogo kwenye Jimbo la Muhambwe Mkoani Kigoma wakati Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa alipozindua kampeni hizo kwenye uwanja wa Taifa wa Kibondo, Mei 4, 2021. Jamal alikuwa ni mmoja wa wagombea wenye ushawishi mkubwa katika kura za maoni za wana CCM waliowania uteuzi wa kupeperusha bendera ya Chama chao kwenye Jimbo hilo
Mmoja kati wanachi wengi wa Kibondo waliojitokeza kumsikiliza Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa wakati alipozindua kampeni za CCM katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Muhambwe Mkoani Kigoma kwenye Uwanja wa Taifa wa Kibondo, Mei 4, 2021. Dkt. Florence Samizi ndiye mgombea wa CCM katika jimbo hilo.
No comments:
Post a Comment