Habari za Punde

Wakazi wa Nyanda za Juu Kusini Watakiwa Kutangaza Vivutio vya Utalii Walivyonavyo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (wapili kulia ) akikimbia mbio za kilomita tano akiwa  pamoja na baadhi ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mbeya wakati wa Tamasha la  Tulia Marathon (MTM) lililofanyika leo  kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja akipokea zawadi kutoka kwa  Katibu wa Kamati ya Olympic Tanzania (TOC),  Philbert Bai iliyotolewa na Kampuni ya Silent Ocean mara naada ya kumaliza kukimbia mbio za kilomita tano katika Tamasha la Mbio za Tulia Marathon lililofanyika mapema leo jijini Mbeya. Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Eng. MaryPrisca Mahundi na Katikati ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Geku
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (wa nne kushoto) akiwa amevaa Medali  huku akiwa ameishika mkononi aliyokabidhiwa mara baada ya kumaliza mbio za kilometa tano ambazo alikimbia wakati wa Tamasha la Mbio za Tulia Marathon zilizofanyika leo Jijini Mbeya.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe Mary ,Masanja (kushoto) akizungumza  jambo na Millard Alfrael Ayo wakati wa Tamasha la Mbio za Tulia ( MTM) zilizofanyika leo jijini Mbeya. Wakwanza Kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Tulia Trust, na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja amewataka wakazi wa Nyanda za Juu Kusini kutambua na kutangaza vivutio vya Utalii vilivyomo katika maeneo yao.


Akizungumza na wakazi wa jiji hilo wakati wa  Tamasha la Tulia Marathon lililofanyika  jijini humo Mhe, Mary Masanja amesema sehemu kubwa ya sekta ya Maliasili na Utalii ni kuhamisha wakazi wote kuvitambua vivutio vyao vya Utalii;

"Kama sekta ya Maliasili na Utalii sehemu yetu kubwa ni kuhamasisha wanambeya, wanakanda ya nyanja za juu kusini kuvitambua vivutio walivyonavyo katika maeneo yao, sisi tunahamasisha Utalii wa ndani kupitia vivutio tulivyonavyo"

Aidha amesema kuwa nyanda za juu kusini hasa jijni la mbeya  kuna vivutio vingi na hivyo inapaswa vitangwazwe kwani maeneo hayo yanahamasisha utalii wa ndani na nje ya nchi;

 "Tuna Msitu wa Asili wa Rungwe ,tuna Ziwa Kingosi ,tuna Hifadhi ya Ruaha , tuna kimondo kwahiyo haya maeneo yote kwa Nyanda za juu Kusini ni maeneo mazuri ambayo yanahamasisha Utalii wa ndani na wa nje ya nchi" amesema Mary

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.