Habari za Punde

Madiwani na Wafanyakazi wa ZECO na ZAWA Wapatiwa Elimu ya Haki na Wajibu wa Mtumiaji.

AFISA Elimu na uhamasishaji kutoka baraza la kuwawakilisha watumiaji wa huduma za maji na nishati Zanzibar (CRC) Ndg.Khamis Ame Mnubi, akiwasilisha mada juu ya haki na wajibu wa mtumiaji kwa madiwani na watendaji kutoka ZAWA na ZECO, hafla iliyofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Micheweni.
KATIBU Mtendaji wa baraza la kuwawakilisha watumiaji wa huduma za maji na nishati Zanzibar(CRC), Hadia Abdul-rahman Othaman, akiwasilisha mada juu ya kujuwa umuhimu wa baraza la kuwawakilisha watumiaji wa huduma za maji na nishati, kwa madiwani wa wilaya ya Micheweni na watendaji kutoka ZAWA na ZECO, hafla iliyofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Micheweni.

BAADHI ya madiwani kutoka wilaya ya Micheweni na watendaji kutoka ZECO na ZAWA, wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa mada mbali mbali, kutoka kwa watendaji wa baraza la kuwawakilisha watumiaji na huduma za maji na nishati (CRC) Zanzibar, hafla iliyofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Micheweni.

(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.