Habari za Punde

Mashamba 263 ya Wakulima wa Miwa Kupatiwa Hati za Hiliki za Kimila Kijiji cha Mkundi na Kilosa.

Diwani wa Kata ya Dumila, Douglas Mwigumila akioa shukrani kwa uongozi wa Mkurabita kwa kazi nzuri ya urasimishaji mashamba ya wakulima wa miwa katika Kijiji cha Mkundi.
Afisa Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa,Robert Lyanzile aktoa mafunzo kuhusu umuhimu wakulima hao kuanzisha chama chao cha ushirika ili mambo yao yawe yanakwenda vizuri ikiwemo kupata mikopo kwa urahisi.
Afisa Mahusiano Biashara wa Benki ya CRDB Tawi la Kilosa, Joel Danford akielezea umuhimu wa kujiunga na benki hiyo na jinsi ya kupata mikopo.
Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, Sandabila akielezea faida za urasimishaji ardhi na jinsi ya kuthaminisha mali.
Sehemu ya wakulima wa miwa ambao mashamba yao yamesharasimishwa wakiwa katika mafunzo hayo.
Wakulima wadogo wa miwa katika Kijiji cha Mkundi, Kata ya Dumila, wilayani Kilosa wakifurahia jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo ikiwemo kanuni za kilimo bora cha zao hilo, yaliyoandaliwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania Juni 10, 2021.

Na Richard Mwaikenda, Kilosa

Zaidi ya mashamba 263 ya wakulima wadogo wa miwa katika Kijiji cha Mkundi, Kata ya Dumila, wilayani Kilosa, Morogoro yamerasimishwa kwa lengo la kuyapatia Hati Miliki za Kimila zitakazotumika kuweka dhamana kukopa fedha benki na taasisi zingine za kifedha ili kuboresha mashamba yao na miradi mingine.

Kazi hiyo ya urasimishaji imedhaminiwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita) ambapo upimaji mashamba uliongozwa na Meneja wa Urasimishaji Ardhi Vijijini wa mpango huo, Anthony Temu kwa ushirikiano na maafisa wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa.

Pia, wameendesha mafunzo kwa wanakijiji yanayohusu, kanuni za kilimo bora cha miwa, faida za uanzishwaji wa chama cha ushirika, utunzanji kumbukumbu za mahesabu, uthaminishaji mali, kuchangamkia fursa mbalimbali na faida za kujiunga na benki.

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video ujue yaliyojiri wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika Shule ya Msingi Mkundi Juni 10,2021.......

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.