Habari za Punde

Mashirikiano kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na sekta binafsi yamechangia kuimarika sekta ya Uchumi

Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa wamiliki wa mahotel Zanzibar wakifuatilia hotuba ya Rais iliowasilishwa na Mkamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla alitoa katika hoteil ya Serena Inn Shangani.
Mwenyekiti wa Umoja wa wamiliki wa Mahotel Zanzibar Bw. Paulo Rosso akimshkuru Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kuweka milango wazi katika suala zima la uwekezaji kupitia sekta ya utalii katika hafla iliofanyika hoteil ya Serena Inn Shangani.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akimuwakilisha Rais Dk. Mwinyi katika uzinduzi wa Umoja wa wamiliki wa Mahotel Zanzibar (HAZ) katika hafla iliofanyika hoteil ya Serena Inn Shangani.
 

Na Kassim Abdi, OMPR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk Hussein Ali Mwinyi amesema kuwepo kwa mashirikiano kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na sekta binafsi imechangia kwa kiasi kikubwa kuimarika kwa sekta ya uchumi wa Zanzibar kupitia sekta ya Utalii.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla alisema hayo kupitia hotuba aliotoa kwa niaba ya Rais wa Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi katika uzinduzi wa Mkuta537no wa umoja wa wamiliki wa Mahoteli Zanzibar hafla ambayo imefanyika katika Hoteli ya Serena Inn Iliopo Shangani.

Alisema kuwepo kwa mashirikiano hayo baina serikali na Sekta binafsi kumepelekea kukuwa kwa Sekta ya Utalii nchini akitolea mfano kuongezeka kwa idadi ya Hoteli kutoka 509 mwaka 2018  hadi kufikia hoteli 620 mwaka 2021 zikiwemo hotele zenye hadhi ya nyota tano.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema uzinduzi wa umoja huo wa wamiliki wa mahotel Zanzibar inadhihirisha wazi kukuwa kwa sekta ya utalii Nchini na kuifanya Zanzibar kuwa miongoni mwa nchi zinapokea watalii wengi kutoka mataifa mbali mbali.

Alieleza kukuwa kwa sekta vya utalii kutasaidia pia kuzalisha ajira kwa wananchi wa Zanzibar, hali ambayo itapelekea kusaidia kupunguza tatizo la upungufu wa ajira nchini.

Alisema Serikali ya Awamu ya Nane imeweka milango wazi kwa sekta binafsi kushauri, kusaidia mawazo katika kuona namna bora ya kukuza utalii Nchini ili kuwanufaisha wananchi wake.

Aidha Mhe. Hemed amliutaka Uongozi wa Umoja wa Wamiliki mahotel Zanzibar (HAZ) kuwa na mashirikiano na taasisi nyengine za utalii akitolea mfano Umoja wa watembeza watalii Zanzibar (ZATO) katika kutangaza utalii wa Zanzibar na vivutio vyake.

Nae Mwenyekiti wa Umoja wa wamiliki wa mahoteli Zanzibar Bwana Paulo Rosso alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa kuanzishwa kwa umoja huo kumelenga kukuza huduma za hoteli na amemuhakikishia kuwa umoha huo utafanya kazi kwa ushirkiano ili kusaida kupatikana kwa maslahi baina ya pande mbili.

Aidha Bwana Rosso alimpongeza Mhe. Rais Dk Hussein Mwinyi kwa dhamira yake ya kufungua milango kwa wawekezaji akieleza kuwa hatua hiyo imesaidia kuwapa moyo wawekazaji kuja kuweza Zanzibar.

Kwa upande wake meneja mauzo kutoka banki ya NMB Bwana Albert Mponzi alisema kuwa Sekta ya Utalii ina mchango mkubwa wa kukuza utalii nchini hivyo NMB imepanga kuanzisha huduma ya malipo kwa njia ya mtandao huduma ambayo itawasaidia watalii kufanya miamala kwa njia ya urahisi Zaidi.

Aidha aliupongeza uongozi huo na kuwaahidi mashirikiano  katika kila hali ili kuona wanaisaidia Serikali katika kukuza Sekta utalii Nchini.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.