Habari za Punde

Mhe Othman: Utawala bora na amani ya kudumu ndiyo chachu ya kuwa na maendeleo endelevu Visiwani Zanzibar.

Na Mauwa Mussa Zanzibar

Mjumbe wa Kamati  kuu ya chama cha ACT Wazalendo Othman Masoud Othmani amesema utawala bora na amani ya kudumu ndiyo chachu ya kuwa na maendeleo endelevu Visiwani Zanzibar.

Kauli hiyo aliitoa  Beit-Yamin Malindi Zanzibar  ikiwa ni siku ya mwisho ya ziara  iliondaliwa na chama hicho kwa ajili ya kumtambulisha kwa viongozi wa Mikoa, Majimbo, na  Matawi kwa upande wa Unguja.

Alisema Kama Zanzibar itakuwa na utawala bora na amani yenye kuendelea ni rahisi kuwa na mabadiliko makubwa ya kimaendeleo kwa muda mfupi kwa kile alichokieleza wawekezaji kuvutiwa na hali hiyo.

Tukiwa utawala bora utaona wawekezaji watakavyomiminika kwani wanauhakika na watakachokiwekeza kuwa kipo katika mikono salama” alisema Othman.

Mjumbe huyo ambae pia ni Makamo wa Kwanza wa rais wa Zanzibar alisema nchi nyingi Ulimwenguni zimekuwa zikiendelea kwa haraka kwa sababu ya uwepo wa utawala bora ambao umeweka misingi ya kila sekta.

Aidha alisema mwaka 1964 wazee walifanya mapinduzi wakiwa na dhamira ya  kubadilisha mfumo wa utawala na kuwa utawala ambao utafurahiwa na raiya pamoja na wageni.

Alisema  wazee walipindua  kuondosha umaskini na kusimamiasha utawala bora ambalo ameahidi kulisimamia ili watu kuwajibika katika majukumu yao.

Alisema uwepo wa Utawala bora ndio itakayopelekea kuendesha uchaguzi kwa misingi ya sheria na kuheshimu maamuzi ya waliopiga kura.

“Utawala bora ndio pekee utakaotuletea uchaguzi bora na kuendeleza amani yetu tulinayo” alisema Othman.

Aidha alisema katika hili wamejitolea kuungana pamoja kuingia kwenye serikali ya Umoja wa kitaifa (JNU) si kwa ajili ya kutafuta vyeo bali ni kwa lengo la   kuleta utawala bora ambao utakuwa wepesi kwa maendeleo ya kweli nchini.      

Mapeema Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho kwa upande wa Zanzibar Juma Duni Hajai alisema dhana ya utawala bora ndio njia pekee ya kuwa na  Umoja wa kitaifa wenye maslahi na taifa. 

Sambamba na hilo aliwataka wananchi waendeleeze amani iliopo ili iwerahisi kwa wawekezaji kuingia nchini na kueleze kuwa ndio  njia ya wananchi kupata ajira kwa ajili ya kuendesha maisha yao.

“Hakuna asiyejua maisha yetu ni magumu kila sehemu lakini tukiwa utawala ambao unawajali watu itakuwa rahisi kutoka katika hali hiyo”.

Sambamba na hilo Makamu aliwataka wanachama wa chama hicho kumpokea na kumuamini Kiongozi huyo ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.