Msanii wa Bongo Flava Chege akitowa burudani wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Michezo la UMISETA Mkoani Mtwara, akiwa jukwaa akitowa burudani wakati wa hafla hiyo.
Na John
Mapepele, Mtwara
Wasanii
mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya, wakiongozwa na Maua Sama na Chegi wamekonga
nyoyo za wanamichezo wa UMISSETA na kuleta hamasa kubwa kwa wanamichezo na wadau
mbalimbali wa mkoa wa Mtwara walipotumbuiza jukwaani leo Juni 2021 kwenye ufunguzi
wa Mashindano ya Michezo na Taaluma kwa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA)
yaliyofunguliwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa
Caroline Nombo kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Katika ufunguzi
wa leo wa UMISSETA vikundi mbalimbali vya kwaya na ngoma vimetumbuiza na
kuufanya umati wa watazamaji kupanda jukwaani na kuimba pamoja na wasanii
mbalimbali waliokuwa wakitumbuiza.
Akisoma
hotuba ya ufunguzi wa mashindano hayo Profesa Nombo amepongeza ubunifu wa
waandaji wa mashindano ya mwaka huu kwa kuwashirikisha wasanii ili kuja kutoa
burudani katika kipindi cha mashindano haya na kuonesha vipaji na vipawa walivyopewa
na Mwenyezi Mungu.
“Pia ninawashukuru na
kuwapongeza wasanii mbalimbali wanaoendelea kusherehesha wakiwemo Maua Sama na
Chege. Wanahabari na wasanii hawa wanasaidia kuitangaza michezo hii na wameongeza
hamasa kwa jamii kuifuatilia nchi nzima wakiwemo wazazi, walezi wa wanafunzi na
Viongozi wa Vyama vya Siasa na viongozi wa Serikali popote walipo”. Aliongeza
Profesa Nombo
Profesa Nomba alitumia ufunguzi
wa mashindano haya kuwaagiza wadhibiti ubora wa Shule kote nchini kuanzia ngazi ya wilaya, kanda na Makao makuu
ya Wizara kufanya tathmini na kutoa ushauri wa
kuimarisha ufundishaji wa michezo, elimu kwa michezo na sanaa katika
taasisi zote hapa nchini
Amesema katika kipindi hiki Serikali
itaendelea kuhakikisha kuwa shule zinatenga maeneo maalum kwa ajili ya michezo
na Sanaa ili kuibua na kuendeleza vipaji vya wanafunzi.
Amesisistiza kuwa michezo ya
UMISSETA na ile ya vyuo vya ualimu
(UMISAVUTA) imekuwa ikiibua vipaji vya wanamichezo wengi ambao miongoni mwao
wamefanikiwa kung’ara kitaifa na kimataifa ambapo amesema kutokana na hilo
Serikali imeamua kurejesha mashindano yaVyuoi vya Ualimu pia kwa kuzingatia agizio
la Mkuu alilolitoa mwaka 2019 wakati
wa kufungua mashindanio ya UMISSETA na UMITASHUMTA la
kutaka mashindano hayo yarejeshwe.
Aidha amesema wachezaji wenye
mafanikio duniani ni wale wenye nidhamu viwanjani na nje ya uwanja na kuwataka
wanamichezo wote kuwa na nidhamu ili kufika katika kiwango cha juu.
“ Mfano wa wachezaji hao ni Mbwana
Samatta, Hashimu Thabiti, Saimoni Msuva, Usain Bolt Lionel Messi,
Christian Ronaldo na wengine wengi . ni matarajio ya kila mmoja wetu kuona
mkishindana kwa ujuzi na maarifa ya hali ya juu ili kupata washindi mahiri
wenye vigezo vya kuweza kushindana kitaifa na kimataifa” alifafanua
Mashindano
yameandaliwa na Wizara tatu zinazohusika na Elimu, Michezo na TAMISEMI chini ya
Kamati ya Uratibu ya Kitaifa ya Makatibu Wakuu wa Wizara hizo.
Mashindano
haya yalitanguliwa na Mashindano ya Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi
(UMITASHUMTA) yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa Juni 8, mwaka huu mjini Mtwara na kufungwa
na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Pauline Gekul
Juni 18, 2021.Mashindano ya UMISSETA yanatarajiwa kufungwa rasmi Julai 3, mwaka
huu.
No comments:
Post a Comment