Habari za Punde

Mbunge wa Jimbo la Kojani Pemba Mhe.Hamad Hassan Chande Akabidhi Jengo la Madarasa Lenye Vumba Vinne

MBUNGE wa Jimbo la Kojani Kisiwani Pemba na Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Hamad Hassan Chande, akiwauliza swali wanafunzi wa darasa la nne, katika skuli ya msingi kangagani mara baada ya kukabidhi banda jipya la kisasa lenye vyumba vinne vya kusomea.
MBUNGE wa Jimbo la Kojani Kisiwani Pemba  na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Hamad Hassan Chande, akiakagua mitihani ya majaribio ya wanafunzi wa Kidato cha nne skuli ya msingi Kangagani.
MBUNGE wa Jimbo la Kojani Kisiwani Pemba na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Hamad Hassan Chande, akizungumza katika hafla ya kukabidhi banda la kisasa lenye vyumba vinne vya kusomea wanafunzi wa skuli ya msingi Kangagani Wilaya ya Wete, lililojengwa na wafadhili kupitia Mbunge huyo.
BAADHI ya wazazi wa wanafunzi, wajumbe wa kamati ya ujenzi ya skuli ya kangagani na wajumbe wa kamati ya skuli hiyo na wanafunzi, wakimsikiliza kwa makini Mbunge wa Jimbo la Kojani na Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Hamada Hassan Chande, wakati wa hafla ya kukabidhi banda la skuli kwa uongozi wa kamati ya skuli.
WANAFUNZI na wajumbe wa kamati ya skuli na kamati ya ujenzi wa banda moja la skuli lenye vyumba vinne vya kusomea, wakifuatilia kwa makini hafla ya makabidhiano ya jengo hilo, kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Kojani ambaye ni Naibu waziri ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Hamad Hassan Chande,kwenda kwa kamati ya skuli ya msingi Kangani

MBUNGE wa Jimbo la Kojani Kisiwani Pemba na Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Hamad Hassan Chande (katikati), akiitikia dua maalumu iliyoombwa kwa ajili yake na wajumbe wa kamati ya skuli ya Msingi Kangagani, baada ya kuwakabidhi banda la kisasa lenye vyumba vinne vya kusomea wanafunzi.

(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.