Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi awaapisha Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu aliowateua leo Ikulu

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Omar Othman Makungu wakifuatilia kuapishwa kwa Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu walioteuliwa hivi karibuni, na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) hafla ilifanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
BAADHI ya Wanafamilia wakihudhuria hafla ya kuapishwa kwa Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu, walioteuliwa hivi karibuni na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa amesimama wakati ukipigwa wimbo wa Taifa wa Tanzania na wa Afrika Mashariki kabla ya kuaza kwa kuwaapisha Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu aliowateua hivi karibuni, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa amesimama wakati ukipigwa wimbo wa Taifa wa Tanzania na wa Afrika Mashariki kabla ya kuapishwa kwa Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu wa Wizara za SMZ katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar, aliowateua hivi karibuni na (kulia kwa Rais) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Ndg Mussa Haji Ali kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, hafla hiyo ya kuapishwa imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Ndg.Issa Mahfoudh Haji kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ,hafla hiyo ya kuapishwa imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Dkt.Habiba Hassan Omar, kuwa Katibu Mkuu Ofisi Kazi Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, hafla hiyo ya kuapishwa imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Ndg.Mikidadi Mbarouk Mzee, kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ,hafla hiyo ya kuapishwa imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Ndg.Aboud Hassan Mwinyi, kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Fedha na Mipango Zanzibar Anayeshughulikia (Fedha na Mipango) hafla hiyo ya kuapishwa imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
BAADHI ya Mawaziri wa SMZ na Viongozi wa Serikali na Dini wakifuatilia hafla ya kuapishwa kwa Makatribu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani)  katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar wakati wa hafla hiyo iliofanyika leo.
WAKUU wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar wakifuatlia hafla ya kuapishwa kwa Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu wa SMZ, wakiapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali waliokaa  na waliosimama ni Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu baada ya kumaliza kuwaapisha katika ukumbi wa Ikulu leo 12-7-2021.(Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.