Habari za Punde

Uzinduzi wa Kituo cha Kisasa cha Kukusanya Taarifa ya Hali ya Hewa Mkanyageni Mkoani Pemba.

MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud, akisalimiana na watendaji mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa na kaimu Mwakilishi mkaazi wa UNDP Tanzania, kabla ya kuzindua kituo cha kisasa cha kukusanyia taarifa za Hali ya Hewa Mkanyageni Wilaya ya Mkoani Pemba
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kifaa cha kisasa cha kukusanya taarifa za hali ya hewa, kilichojengwa kwa ufadhili wa UNDP Tanzania, huko skuli ya Mohamed Juma Pindua Mkanyageni Wilaya ya Mkoani
MKURUGENZI mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa kanda ya Zanzibar Ngwali Mohamed Khamis, akitoa maelezo mafupi kuhusu kifaa cha kisasa cha ukusanyaji wa taarifa za hali ya hewa, kilichojengwa katika skuli ya Mohamed Juma Pindua Wilaya ya Mkoani.
AFISA Ufuatiliaji na Tathmini kutoka UNDP Tanzania Abass katengo akizungumza kwa niaba ya Mwakilishi Mkaazi wa UNDP Tanzania, wakati wa ufunguzi wa kifaa cha kisasa cha ukusanyaji wa taarifa za hali ya hewa, kilichojengwa katika skuli ya Mohamed Juma Pindua Wilaya ya Mkoani kwa ufadhili wa UNDP
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud akizungumza na wananchi na wanafunzi wa skuli ya Mohamed Juma Pindua, mara baada ya ufunguzi wa kifaa cha kisasa cha ukusanyaji wa taarifa za hali ya hewa, kilichojengwa katika skuli ya Mohamed Juma Pindua Wilaya ya Mkoani na UNDP Tanzania
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud akipokea zawadi kutoka kwa Afis ufuatiliaji na Tathmini UNDP Tanzania Abassa Katengo, mara baada ya kumalizika kwa hafla ya uzinduzi wa kifaa cha kisasa cha ukusanyaji wa taarifa za hali ya hewa, kilichojengwa katika skuli ya Mohamed Juma Pindua Wilaya ya Mkoani kilichojengwa na UNDP Tanzania
MUONEKANO wa Kifaa cha kusasa cha ukusanyaji wa taarifa za hali ya hewa, kilichojengwa katika skuli ya Mohamed Juma Pindua Wilaya ya Mkoani kilichojengwa na UNDP Tanzania

MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud kulia, akizungumza na Afis ufuatiliaji na Tathmini UNDP Tanzania Abassa Katengo, kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Viongozi wakuu wa Kitaifa ya BLW Hassan Khamis Hafidhi.

(PICHA NA ABDI SULEIMAN,PEMBA)

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.