Habari za Punde

Uzinduzi wa Mitambo ya FM KIsaki ni utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa

Na.Adeladius Makwega.  Kisaki – WHUSM

Serikali imezindua mitambo ya kurushia matangazo ya Freguence Modulation (FM) hapa Kisaki Mkoani Morogoro ambapo uzinduzi huo umewashirikisha mawaziri wawili wa serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ambao ni Mheshimiwa Innocent Bashungwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo na Mheshimiwa Dkt  Faustine Ndugulile Waziri wa  Mawasiliano na Tekinolojia ya Habari.

 

Shughuli hii pia imewakutanisha watendaji wa taasisi kadha zinazosimamiwa na mawaziri hao, Mheshimiwa Bashungwa anasimamie kile kinachotakiwa kwenda hewani yaani maudhui na mwenzake  Dkt Ndugulile  anasimamia uwezeshaji wa kile kinachokwenda hewani kuweza kumfikia  Mtanzania aliyepo Kiteto, Kisaki, Mahenge, Mpanda, Ndandahimba na maneeo mengine ya Tanzania.

 

Katika uzinduzi huu wa Julai 30, 2021 tumeshuhudia Mkurungezi wa Ufundi wa Shirika la Utangazaji Tanzania mwanamama, Injini Upendo Mbele akitoa maelezo ya kina ya namna mitambo unavyofanya kazi na faida yake kwa sasa.

 

Kando  ya maboresho yote yanayofanywa na serikalikwa TBC, kumekuwa na hoja moja kubwa iweje  kwa sasa serikaili inawekeza upya katika usikivu wa TBC? Mbona hapo awali Redio Tanzania Dar es Salaam ilikuwa ikisikika nchi nzima? hata wapigania uhuru  na katika harakati za ukombozi  redio hii ilifanya kazi kubwa na matangaza  hayo yaliweza kusikika hadi Uganda na mataifa mengine ya Afrika? iweje leo hiii iwe vinginevyo?

 

Kuyajibu maswali hayo nilimsogeza chemba Injinia Upendo Mbele ambaye ndiye  mjuzi  wa masuala ya  kiufundi wa Shirika  la Utangazaji Tanzania (TBC) kwanza alisema kuwa sasa  ni wakati wa  digitali  na haya  matangazo yake  yana ubora mkubwa kuliko yale ya Amplitude Modulation(AM),Short Wave(SW) na Medium Wave (MW). AM,SW na MW ndiyo yaliyokuwa yakitumiwa na Redio Tanzania Dar es Salaam.

 

Kwa sasa vifaa vyake havitengenezwi tena ndiyo maana ili kuweza kuwa na matangazo bora yenye usikivu mkubwa yanayoweza kwenda mbali lazima tutumie mitambo ya FM na ya kidigitali na si vinginevyo.

 

“Ni kweli hapo awali ulifanyika uwekezaji mkubwa kwa wakati huo na ndiyo soko lilikuwa na  vifaa vya AM,SW na MW lakini sasa  soko linatupeleka katika FM na ndiyo maana  hakuna namna lazima twende huko na ndilo linalofanywa na serikali” Alisema Injinia Upendo Mbele.

 

Kwa sasa unapokwenda sokoni kununua vifaa unakutana na vifaa vya FM na siyo vifaa   vya AM, SW na MW. Sisi kama shirika lazima tuweze kuwafikia Watanzania popote waliopo na ndiyo maana tunaongeza wigo wa usikivu wetu, aliongeza Mkurugenzi huyo wa Ufundi wa TBC na ndiyo maana sasa TBC unaweza kuitazama na kuisikiliza hata kama upo Amerika.

 

Kwa mfano wa kawaida wa kawaida tunaweza kusema kuwa ni sawa na mtu ambaye hapo awali aliweza kununua Redio Pleya na ana sanduku kubwa la santuri  zake za zamani. Redio Pleya yake kwa sasa imeharibika na inamsumbua kupata baadhi ya vifaa  hivyo ili kuweza kufanya kazi vizuri.

 

Je afanyaje na  wakati  yeye anashida ya kuusikiliza muziki? ni wajibu wa ndugu yetu huyu kwenda na wakati  anatakiwa kununua vifaa vya kisasa ili aweze kusikilia muziki huo. Vinginevyo TBC haitoweza kusikika na Watanzania watakosa habari za kiuchumi, kibiashara, kilimo na mengine mengi.

 

Hicho ndiyo kilichofanywa na mheshimiwa Bashungwa na Mheshimiwa Ndungulile.

 

Kumbuka kuwa wakati wa harakati za ukombozi ilitumiwa mitambo ya MW, AM,na SW ambayo ilisaidia kufanikisha ukombozi wa bara la Afrika. Nina imani kuwa kwa sasa mitambo hii ya kisasa ya FM itasaidia mno kuleta ukombozi mkubwa wa kiuchumi kwa  maendeleo ya  taifa letu. Kwa maana mkoloni wa sasa ni njaa, umasikini, maradhi na ujinga.

 

Mheshimiwa Bashingwa na  mwezake Mheshimiwa Ndungulile  pamoja na watumishi wote wa Wizara zote mbili za Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo na Wizara ya  Mawasiliano na Tekilonojia ya Habari wanapaswa kupongezwa mno kwa kutimiza wajibu wao kwa manufaa ya taifa letu.

 

Wananchi kwa upande wao wana wajibu wa kuitunza mitambo hii ambayo ipo katika maeneo yao kama serikali ilivyosema na kuungwa mkono na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigella akisema kuwa wao watahakikisha mitambo hiyo inakuwa salama na ikiendelea kufanya kazi.

 

“Wananachi wa Maorogoro wanatambua umuhimu wa mitambo hii na ndiyo maana wnaomba makampuni ya simu yake kuweka vifaaa vvyao ili waweze kupata mawasiliano ya simu. Ndiyo maana leo hii wmaejitokeza kwa wingi nawahakikishia kuwa mitambo hii ipo sehemu salama.” Alisema Mkuu  huyo wa Mkoa wa  Morogoro.

 

“Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa Miaka mitano 2020/2021-2025/2026 umeainisha vipaumbele  vya TBC  ni uwekezaji wa miundo mbinu ya utangazaji, ikiwamo upanuzi wa usikivu wa redio pamoja na miundo mbinu yake.” Na hili ndilo lililofanyika Kisaki. Alisema Mheshimiwa Bashungwa Waziri wetu wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

 

Naweka kalamu yangu chini kwa muda huu ili niweze kuanza safari yangu ya kurudi Morogoro mjini na kwa sasa nikisikiliza Redio za TBC Taifa na TBC FM zikikata mawimbo vizuri hapa Kisaki.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.