Habari za Punde

Wabunge Watembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro.

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiangalia nyayo za binadamu wa kale zilizoko Olduvai Gorge katika Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro walipofanya utalii wa ndani katika eneo hilo jana.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akitoa ufafanuzi kuhusu utunzaji wa fuvu la binadamu wa kale lililoko Olduvai Gorge kwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro walipofanya utalii wa ndani kwenye eneo hilo jana.
Afisa Mambo ya Kale, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Godfrey Ole Moita (kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu mchanga  unaohama  kwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waliotembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kwa ajili ya utalii wa ndani wakiongozwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (wa nne kushoto) jana.
Afisa Mambo ya Kale, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Godfrey Ole Moita (kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu chanzo cha Olduvai Gorge  kwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waliotembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kwa ajili ya utalii wa ndani wakiongozwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (wa pili kushoto) jana.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.