Habari za Punde

Wananchi wa Kijiji cha Kobokoni Kisiwani Pemba Wawataka Mwakilishi na Mbunge Kumalizia Ujenzi wa Skuli ya Maandalizi.

MWAKILISHI wa Jimbo la Wawi Wilaya ya Chake Chake Mhe.Bakari Hamad Bakari, akizungumza na wananchi wa Kibokoni Vitongoji mara baada ya kukagua ujenzi wa skuli ya maandalizi Kobokoni, ambayo inahitaji kuezekwa kwa sasa kupitia mwakilishi na Mbunge wa jimbo hilo.
WANANCHI wa shehia ya kibokoni Vitongoji wakimsikiliza kwa makini Mwakilishi wa jimbo la Wawi Wilaya ya Chake Chake, wakati alipofika kukagua ujenzi wa banda la skuli ya maandalizi kibokoni, ambayo imo katika mkakati wa kumaliziwa ujenzi wake na mwakilishi wa jimbo hilo
BAADHI ya wajumbe wa kamati ya jimbo la Wawi Wilaya ya Chake Chake wakikagua, skuli ya maandalizi Kibokoni Vitongoji skuli hiyo tayari imeshapangwa na kamati hiyo kumalizwa ujenzi wake, kupitia mwakilishi na mbunge wa jimbo hilo
MWAKILISHI wa Jimbo la Wawi Wilaya ya Chake Chake Mhe.Bakari Hamad Bakari, akikagua banda la skuli ya maandalizi Ditia Jimbo la Wawi, kwa ajili ya kufanyiwa matengenezo makubwa hadi kukamilika kwake, baada ya kupitishwa na kamati ya jimbo.
(PICHA NA ABDI 
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.