Habari za Punde

Wananchi Watakiwa Kuendelea Kuchukua Tahadhari Juu ya Maambukizi ya Covid 19. Mhe.Hemed

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na waumini wa Masjid Shifaa uliopo Muembetanga mara baada ya kukamilika kwa ibada ya sala ya Ijumaa.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla alijumuika na waumini wa Masjid Shifaa Muembetanga Jijini Zanzibar katika Ibada ya Sala ya Ijumaa, ambapo amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadahri juu ya maambukizi ya ugonjwa wa covid 19 kwa kufuata maelekezo ya Wataalamu wa Afya.

Nae, Khatibu wa Msikiti huo Ustadh Nassir Ali Haji amewakumbusha waumini wa dini ya Kiislamu kuendelea kuliombea taifa ili kukingwa na maradhi mbali mbali yakiwemo maradhi ya mripuko

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.