Habari za Punde

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango afanya ziara katika Taasisi zinazotoa Huduma Bandarini Zanzibar

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar Jamal Kassim Ali akizungumza na Naibu Kamishna wa TRA Kituo cha Bandarini Sheikha Said Ali kuhusu kuboresha huduma kwa wateja katika ziara yake aliyoifanya Bandari Malindi Mjini Zanzibar.

Mkurugenzi huduma za Bandari na Uendeshaji Muhandisi Mansour Rashid akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,  Fedha na Mipango Zanzibar Jamal Kassim Ali kuhusu huduma wanazotoa bandari wakati wa ziara yake.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar Jamal Kassim Ali akiwa na watumishi wa wizara yake na watumishi wa bandarini wakikagua maeneo mbalimbali ya yanayotoa huduma bandarini katika ziara yake ya kwanza tokea kuanza kwa mwaka mpya wa fedha.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar Jamal Kassim Ali akizungumza na wandishi wa Habari mara baada ya kumaliza ziara yake katika Bandari ya Malindi Mjini Zanzibar.

Picha na Makame Mshenga.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.