Habari za Punde

Chanjo ya Uviko 19 yaziduliwa Tabora

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Batrida Buriani akizindua zoezi la Chanjo ya Uvico 19 kwa Wananchi wa Mkoa wake leo katika ukumbi wa Isike Mtemi Mwanakiyungi Mkoani Tabora.  

Na Lucas Raphael,Tabora

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt Batrida Buriani amepiga marufuku Hospitali yeyote ya Umma au binafsi kuwalipisha wananchii gharama katika zoezi la Chanjo ya Uvico 19  na lifanyike kwa uadilifu na kwa haki kwa walengwa.

 

Aliyasema hayo kwenye hotuba yake katika uzinduzi wa Chanjo hiyo kwenye Ukumbi wa Isike Mtemi Mwanakiyungi Mkoani Tabora ambao ulihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa wakuu wa idara, waganga wakuu wa halmashauri, wakuu wa wilaya na kamati ya ulinzi na Usalama.

 

Alisema Mkoa wa Tabora unatarajia kutoa Chanjo ya Uvico19 kwa wananchi wapatao 30, 000 katika halmashauri 8 kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassani kufanikisha upatikanaji wa chanjo hapa nchini.

 

Mkuu huyo wa mkoa alisema uzinduzi huo unatoa fulsa kwa wananchi ambao wapo tayari kuchanjwa ili kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa wa Covid 19 , pamoja na kupunguza hatari ya kupata madhara makubwa endapo mtu atapata maambukizi.

 

Aidha alisema  kwamba Mkoa wa Tabora umeanza zoezi hilo leo Aagosti 3 2021 katika vituo vilivyoainishwa ambavyo ni 3 kwa kila halmashauri na kufanya mkoa kuwa jumla ya vituo 24 .

 

Hata hivyo alisema kwamba wananchi walio tayari kuchanjwa watajisajili latika mfumo wa Taifa ama katika vituo vilivyochaguliwa  katika halmashauri husika na kupatiwa cheti baada ya kuchanjwa.

 

Alitoa wito kwa wanahabari, wananchi , viongozi wa jamii na viongozi wa madhehebu mbalimbali na wengine wahakikishe wanapeleka ujumbe kuhusu huduma za chanjo kuwaelimisha na kuwaelekeza wananchi kwenda kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.

 

Kwa Upande wake Mganga Mkuu Mkoa Honoratha Rutatinisibwa alitoa taarifa kwamba chanjo zimepunguza magpnjwa mengi ambayo yalikuwa yanasumbua jamii na yalizoea kuuwa watu wengi lakini kwa sasa baadhi ua magonjwa hayo hayaonekani.

 

Rutatinisibwa alisema kwamba takwimu za shirika la afya Duniani (WHO) zinaonyesha hadi kufikia agost 2 mwaka huu kulikuwa na idadi ya wagonjwa walioathirika duniani koye ni 198, 234, 951 na vifo 4, 227, 357 ma kiasi cha dozi chanjo za UVICO 19 zilizokuwa zimetolewa duniani kote 3, 839, 816, 037 ili kupambana na ugonjwa huo.

 

Alisema kwamba faida za chanjo za ugonjwa UVICO 19 tafiti zilifanyika katika nchi mbalimbali ambapo chanjo zimekwishatolewa kwa kiwango cha juu  kama Uingereza (UK) Israelna na Qatan ambazo zinaonuesha matokeo mazuri ya kupunguza kiwango cha maambukizi.

 

Alifafanua kwamba tafiti zinaonyesha ukipata chanjo hiyo , unaweza kupata maambukizi ya ugonjwa huo , Lakini hautapata ugonjwa mkali wa kukufanya kufikia hadi kulazwahospitalini kuongezea hewa ya Oxgen au kufa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.