Habari za Punde

Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) watakiwa kujikomboa kiuchumi

Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Sharifa Omar Khafan akipata maelezo kutoka kwa wajasiriamali wa Mkoa wa Mjini Kichama juu ya bidhaa wanazozizalisha wakati akiyakagua maonesho ya Wajasairiamali hao.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Sharifa Omar Khafan akipata maelezo kutoka kwa wajasiriamali wa Mkoa wa Mjini Kichama juu ya bidhaa wanazozizalisha wakati akiyakagua maonesho ya Wajasairiamali hao.
Wajasiriamali wanawake wa Mkoa wa Mjini wakiskiliza Hotuba ya Mgeni Rasmi Mama Sharifa Omar Khalfan Wakati akifungua Mkutano wa Wajasiriamali wanawake wa Mkoa Mjini uliofanyika katika Ukumbi wa CCM Amani Mkoa.


 Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Sharifa Omar Khalfan akizungumza na Wajasiriamali wa Mkoa wa Mjini Kichama wakati akifungua Mkutano wa Wajasiriamali hao ambapo aliwasisitiza kuendelea kujikomboa Kiuchumi.

Na Kassim Abdi, OMPR

Mke wa   Makamu wa Pili wa Rais Mama Sharifa Omar Khalfan amewataka wanachama wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) kuendelea kujikomboa kiuchumi kwa kutumia njia bora  za kujipatia kipato.

Mama Sharifa Omar Khalfan alileza hayo wakati akifungua rasmi mkutano wa wajasiriamali wanawake wa Mkoa wa Mjini kichama uliofanyika katika Ukumbi wa CCM Amani Mkoa.

Alisema umefika wakati kina mama kujikwamua kiuchumi wakizingatia kwamba Jumuiya hiyo imepewa jukumu la kumkomboa Mwanamke kiuchumi ,kisiasa na kijamii.

Alieleza kuwa, ni vyema kwa washiriki wa mafunzo hayo kusarifu bidhaa zao kwa lengo la kuzipandisha thamani ili ziuzike katika soko la Kitaifa na Kimataifa, kwa lengo la kutanua wigo katika kukuza biashara za wajasiriamali.

Mama Sharifa alisema hatua hiyo ni kuunga mkono  jitihada za Serikali katika kuwawezesha wananchi wake kiuchumi, kama ilivyoelezwa katika Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025.

Akigusia kuhusiana na mporomoko wa maadili Mama Sharifa Khalfan aliwataka wazazi na walezi kushirikiana kwa pamoja katika kuyakemea maovu katika ngazi ya familia na jamii kwa ujumla.

 Nae, Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Taifa Ndugu Thuwayiba Kisasi alieleza kuwa mafunzo hayo yatawawezesha kina mama hao kuweza kuendana na maendeleo ya Sayansi na Teknolojia ili kuweza kuboresha bidhaa zao ziweze kuuzika Kitaifa na Kimataifa

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzani Ndugu Tunu Juma Kondo alieleza kwamba kuwepo kwa Mkutano huo ni kuunga mkono juhudi za Serikali pamoja na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kumuinua mwanamke kiuchumi

Pia aliwashajihisha  wajasiriamali wanawake kuacha kutegemea badala yake wajenge uthubutu kwa kuzalisha ili kujiingia kipato jambo ambalo litakalowasaidia kuendesha familia zao.

Mapema Mama Sharifa Omar Khalfan alikagua maonesho ya wajasiriamali wanawake kutoka majimbo Tisa ya Mkoa wa Mjini ili kujionea bidhaa zinazozalishwa na Wajasiriamali hao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.