Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi imeishaurI Wakala wa Serikali
Mtandao Zanzibar (eGAZ) kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kufikia
azma ya kuwa kitovu cha utaalamu na ubunifu katika kuandaa sera, viwango na
taratibu nyengine kwa ajili ya kuimarisha matumizi ya tehama nchini.
Wajumbe wa Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Mhe Ali Suleiman Ameir wametoa
ushauri huo mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa wakala wa serikali
mtandao kwa kipindi cha julai 2020 – juni 2021 katika kikao kilichofanyika katika
ofisi ya wakala hio huko Mazizini.
Wamesema Serikali pamoja na wananchi wanaitegemea sana wakala hio
kutokana na umuhimu wake mkubwa katika mapinduzi ya matumizi ya teknolojia
ambapo ni wajibu kuhakikisha mifumo yao wanaiimarisha na kuiendeleza kwa mujibu
wa sera, viwango pamoja na kutumia mifumo sahihi ya tehama kwa urahisi nchi
nzima .
Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Serikali Mtandao Zanzibar,
Said Seif Said akiwasilisha taarifa ya utekelezaji kwa kipindi cha
julai 2020 –juni 2021 ameielezea kamati hiyo kwamba serikali
mtandao ina fursa kubwa ya kuleta mabadiliko katika utendaji wa kazi serikalini
na kutoa huduma bora pamoja na kuongeza wingi wa ukusanyaji wa mapato.
No comments:
Post a Comment