Habari za Punde

Kamati ya Mawasiliano,Ardhi na Nishati ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Yatembelea Bandari Mkokotoni na Wizara ya Maji

Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano, Ardhi na Nishati ya Baraza la Wawakilishi Mhe.Yahya Abdallah Rashid akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Maji Nishati na Madini (kushoto) Waziri wa Wizara hiyo Mhe Suleiman Masoud Makame, mkutano huo wa Kamati umefanyika katika ukumbi wa Ofisi hiyo Maisara Suleiman Jijini Zanzibar.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano, Ardhi na Nishati Mhe Yahya Abdallah Rashid akitoa ushauri kwa uongozi wa Wizara ya Maji, Nishati na Maadini mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara hiyo kipindi cha April / Juni 2020/2021, (kushoto) Waziri wa Maji, Nishati na Madini Zanzibar Mhe.Masoud Suleiman Makame na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt.Mngereza Mzee Miraji.
Wajumbe wa Kamati ya Mawasiliano, Ardhi na Nishati ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakitembelea Mradi wa ujenzi wa Bandari ya Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja na kupokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Bandari hiyo.
Wajumbe wa Kamati ya Mawasiliano, Ardhi na Nishati wakitembelea na kupokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Bandari ya Mkokotoni.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.