Habari za Punde

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said Awataka Wafanyabiashara katika Eneo la Skuli ya Sekondari Vikokotoni Kuhamisha Biashara Zao Kutowa Nafasi Kwa Wanafunzi.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akiangalia Wafanya biashara wanaoendelea kufanya biashara zao kwenye madirisha ya Skuli ya Sekondari Vikokotoni, kutokana na agizo alilolitoa la kutofanywa biashara katika maeneo hao.

Agizo hilo la Mhe. Simai amelitoa  kutokana na malalamiko ya Wanafunzi wa Skuli hiyo kuwa sauti za wafanya biashara zinawapa changamoto wanapokuwa darasani  kwa kushindwa kushughulikia masomo yao.


Vyombo vya moto vikiwa vimeegeshwa katika eneo la Skuli ya Sekondari ya Vikokotoni.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.