Habari za Punde

Dunia Inakwenda Kasi Juu Mabadiliko na Matumizi ya Teknolojia -Waziri Simai.

Na. Maulid Yussuf WEMA Zanzibar.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe, Simai Mohammed Said amesema Dunia hivi sasa inaenda kwa kasi sana juu ya mabadiliko na matumizi ya Teknolojia.

Amesema Wizara pia imeamua kuhakikisha kuwa katika Skuli zake pamoja na Elimu inayotoa iwe inakwenda sambamba na mabadiliko ya Dunia.

Mhe Simai ameyasema hayo wakati wa hafla ya ufunguzi wa maabara za nishati mbadaka na  mafuta na Geai, katika Ukumbi wa Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia, Mweni Mjini Unguja.

Amesema Wanatambua kuwa nyenzo itakuwa ni changamoto katika Skuli,  lakini safari ni hatua, na hivyo imani yake kuwa mafanikio  yatafikiwa endapo watakuwa na nia na mashirikiano ya dhati katika utekelezaji wa suala hilo.

Amesema Serikali ya awamu ya nane chini ya Uongozi wa Mhe Rais Dkt Hussein Ali Mwinyi inakusudia kuboresha maisha ya Wazanzibari wote na hilo linaonekana katika sera zilizo bora zinazotekelezwa kwa ujumla.

Amesema Serikali inatambua juhudi kubwa inayofanywa na Taasisi hiyo kwa kuwafundisha vijana watakalolisaidia Taifa, kwa kutoa wataalamu wengi wanaokidhi kutatua za changamoto za kiufundi, ndani na nje ya nchi.

Amefahamisha kuwa, kasi ya Taasisi hiyo kuamua kuongeza Fani hizo mbili za Nishati mbadala na Mafuta na Gesi, ni jambo kubwa  na imani yao ni kuendelea kufanya kazi vizuri katika Mazingira Bora.

Mhe Simai, ameipongeza Taasis hiyo kwa utunzaji mzuri wa vifaa vilivyopo tokea mwaka 1967 vya Idara ya uhandisi wa magari ambavyo vipo hadi leo, hivyo amewataka kuendelea kuvitunza na vifaa hivyo vipya ili na wengine waweze kuvitumia.

Hata hivyo amewasisitiza Bodi ya Taasisi hiyo kuendeleza siri na kuheshimu utaratibu wa uongozi, huku akiwataka Wanafunzi kudumisha nidhamu pamoja na kuwa raia wema katika nchi yao.

Aidha amesema Serikali inatoa pongezi kwa wafadhili wa Mradi huo kwa kuchangia kiasi kikubwa cha fedha kwa maendeleo ya nchi, pamoja na kutoa pongezi kwa Taasisi ya Karume, Sayansi na Teknolojia kwa mchango wao Mkubwa wa kuhakikisha ukuaji wa Teknolojia unafikiwa katika nchi.

Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Karume Sayansi na Teknolojia Dkt Afuqa Khalfan Mohammed, amesema uwekezaji wa maabara hizo ni muhimu sana kwa Taaisisi hiyo kwani sasa  utaiweza kutia mafunzo hayo kwa nadharia na vitendo na hivyo kutoa imani kwa wasimamizi na wakufunzi kuwa Wanafunzi watakaomaliza watakuwa waliobobea.

Kwa upande wake Mkurugenzi Taasisi ya Karume, Sayansi na Teknolojia  Dkt Mahmoud Abdulwahab Alawi amesema ufunguzi wa maabara hizo  unatokana na kununuliwa na kuwekwa vifaa vya taaluma ya nishati mbadala na mafuta na gesi ambao umegharimu shilingi milioni 120.

Amesema hatua hiyo imefanyika chini ya Ufadhili wa Tanzania Dutch Energy Capacity Building.

Hata hivyo Mkurugenzi ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Elimu kuwasaidia katika kuwaptia vifaa kadhaa katika nyanja ya mafuta na gesi ili kuweza kutekeleza na kuimarisha vyema sera ya uchumi wa buluu kwa mafanikio ya Taasisi na kuinua uchumi wa nchi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.