Habari za Punde

Maafisa Tehama OMKR watakiwa kuwa wabunifu

Mkurugenzi Mipango Sera na Utafitii Bi Daima M. Mkalimoto akifungua mafunzo kwa maafisa Tehama na wakuu wa vitengo wa Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais 

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya matumizi ya Tehama wakisikilliza kwa makini wakati mafunzo yakiendelea.
Na Raya Hamad – OMKR.
Maafisa Tehama na wakuu wa vitengo wametakiwa kuwa wabunifu na kushirikiana katika majukumu yao ya kazi ili kuendana na kasi ya iliyopo ya ukuwaji wa teknologia ulimwenguni
Mkurugenzi Mipango, sera na utafiti Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Bi Daima Mohammed Mkalimoto ameyasema hayo leo wakati akizindua mafunzo kwa maofisa tehama na wakuu wa vitengo wa ofisi hio na taasisi zilizochini yake kwenye ukumbi wa mkutano wa ofisi hio Migombani.
Amesema serikali mtandao inatakiwa kuwa hai muda wote katika kutoa ushirikiano ili iwe ni suluhisho la kiutendaji katika mabadiliko na kufanya masuala ya tehama kuwa rahisi na kuwa na mfumo mmoja wenye tija kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar .
Nae mkufunzi wa mafunzo hayo Ndugu Ali Abdi Ali kutoka Serikali Mtandao amesema maafisa tehama ili waendane kasi ya mabadiliko ya mawasiliano ni muhimu wawe wanapatiwa mafunzo  ya mara kwa mara jambo ambalo litapelekea kuwa umakini katika utendaji wao wa kazi.
Aidha washiriki wa mafunzo hayo waishukuru Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais na kuomba muendelezo wa mafunzo hayo ili kuwa weledi zaidi na kufahamu maendeleo ya mawasiliano ya tehama.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.