Habari za Punde

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Mlezi wa CCM Mkoa wa Tanga Mhe Hemed Suleiman Akiendelea na Ziara Yake Mkoani Humo.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akitembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa bandari ya Tanga akiwa katika muendelezo wa ziara yake katika Mkoa Huo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga  ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akimuagiza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania kuhakikisha Mamlaka hiyo inaanza kazi ya kuitanga Bandari ya Tanga ili itakapokamilika iweze kutumiwa na watu kutoka Nchi za Jirani.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mlezi wa Chama Cha Mpinduzi Mkoa wa Tanga ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akikabidhiwa zawadi ya msala na Mwenyekiti CCM Shina Nambari Moja Kata ya Usagara, wakati wa ziara yake ya Kichama katika Mkoa wa Tanga.
Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini Mhe. Ummy Mwalimu akilezea mafanikio yaliofikiwa ndani ya jimbo hilo katika mkutano wa majumuisho kufuatia uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Legal Naivera.

Mjumbe wa kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM Taifa ambae pia ni mlezi wa mkoa wa Tanga Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema kukamilika kwa bandari ya Tanga kutasaidia kuimarika kwa sekta nyengine na kuinua uchumi kwa wananchi wa mkoa huo.

Mjumbe huyo wa kamati kuu alieleza hayo wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa bandari ya tanga inayojengwa na kampuni ya china habour

Alieleza kuwa bandari hiyo itakapokamilika itasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza pato la taifa sambamba na kuongeza kipato kwa wananchi wa kipato cha chini wakiwemo mamantilie

Katika hatua nyengine Makamu wa Pili wa Raisi ameugiza uongizi wa mamlaka ya bandari Tanzania kuchukua hatua ya kuitangaza bandari hiyo ili itakapo kamilika wafanyabiashara pamoja na watu kutoka nchi jirani waweze kupitisha mizigo kwa urahisi

Mhe Hemed aliutaka uongozi wa mamlaka hiyo kujenga ushirikiano mzuri na wafanyabiashara kwa kufuata utaratibu na sheria pamoja na kuwaondoshea usumbufu usiokua wa lazima

"Meli hizi zinakwepa kuja kwasababu ya kukimbia usumbu" Alisema Mhe. Hemed

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania Eric Khamis alimueleza Makamu wa Pili wa Rais kuwa ujenzi wa bandari hiyo umejumuisha uchimbaji wa kina cha bahari kwa urefu wa Mita kumi ambayo bandari hiyo itakuwa ukubwa wa mita 450.

Aidha, Mkurugenzi Eric alisema badari hiyo itakapokamilika itakuwa na uwezo wa kushusha mizigo tani Millioni Tatu kwa mwaka ambapo ujenzi wake utagharimu jumla ya Shillingi Billioni Mianne Arubaini hadi kukamilika kwake.

“Bandari hii itakapokamilika itaweza kushusha mizigo ya Nchi za kaskazini ikiwemo Ruwanda na Burundi. Alisema Mkurugenzi Eric

Nae, Meneja mradi kutoka kampuni ya china Hubour LYU WEI alimuhakikishia Mlezi wa Mkoa wa Tanga kuwa kampuni ya itajenga bandari hiyo kwa kuzingatia vigezo na viwango ambapo itakapokamilika itasaidia kutatua changamoto ya kupunguza gharama na muda wa ushushaji wa mizigo.

Akiwa katika ziara hiYo Makamu wa Pili wa Rais alipata fursa ya kusalimiana na wanchi wa shina nambari moja kata ya usagara na alimuagiza mkuu wa mkoa kuipatia ufumbuzi changamoto iliyowasilishwa na wananchi juu ya majengo ya bandari yanayosababisha athari kwa wakaazi wa maeneo hayo.

wakati wa mchana mlezi huyo wa mkoa wa tanga aliwasili katika ukumbi wa mikutano LEGAL NAIVERA kwaajili ya mkutano wa majumuisho uliowashirikisha viongozi na wanachama kutoka ngazi ya shina hadi taifa.

Akizungumza katika Mkutano huo wa Majumuisho Mhe. Hemed aliwataka viongozi hao wa Mkoa wa Tanga kukaa pamoja na kuangalia upya hatua bora za kuchukua ili kuinua kiwango cha elimu kwa wanafunzi mkoa wa Tanga.

Makamu wa Pili wa Rais aliuwagiza uongozi wa Mkoa wa Tanga kuchukua jitihada za makusudi katika kurejesha hadhi ya Mkoa wa Mkoa wa Tanga kwa kuchangia pato la taifa kupitia sekta ya viwanda ambavyo kwa muda mrefu sasa viwanda hivyo vimesitisha uzalishaji hali inayopelekea Mkoa huo kukosa maendeleo ya kiuchumi kwa ajili ya kustawisha maisha ya wananchi.

Kwa upande wao viongozi wa Majimbo Mhe. Ummy Mwali na Mhe. Juma Awesu walimueleza Mlezi wa Mkoa huo kuwa kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Tanga wanampongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa ambae pia ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutoa Fedha kwa ajili ya kueleza sera ya Elimu Bure.

Pia, Viongozi hao walisema wanaridhishwa na jitihada zinazochukuliwa na Rais Samia ambapo katika historia kwa mara ya kwanza viongozi wa majimbo walipo katika Bunge la Jamuhuri ya Tanzania wamepatiwa kiasi kikubwa cha Fedha kwa ajili ya kufanikisha miradi ya maendeleo katika majimbo yao.

Mhe. Hemed amekamilisha ziara yake ya Siku tano Mkoani Tanga na kutembelea Wilaya Tano akiwa mlezi wa Mkoa Huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.