Habari za Punde

Mtanzania Achaguliwa Tamasha la Kimataifa la Filamu za Afrika Nchini Ujerumani.

MTANZANIA mwenye asili ya Zanzibar Muslim Nassor maarufu kama Jazzphaa Jazz anayefanya shughuli zake nchini Ujerumani amechaguliwa kuwa mmoja wa watakaokuwa kwenye tamasha kubwa la Kimataifa la filamu za Afrika, zitakazofanyika Koloni, Ujerumani. 

Na Andrew Chale 

MTANZANIA mwenye asili ya Zanzibar Muslim Nassor maarufu kama Jazzphaa Jazz anayefanya shughuli zake nchini Ujerumani amechaguliwa kuwa mmoja wa watakaokuwa kwenye tamasha kubwa la Kimataifa la filamu za Afrika, zitakazofanyika Koloni, Ujerumani. 

Kwa mujibu wa  Jazz, Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika siku ya Alhamisi tarehe 16 - 26 September mwaka huu.

"Ninayo furaha ya kuwatangazia nimepata kuchaguliwa kuwa mmoja wa watu ambao watatambulisha filamu na kuongoza maongezi ya filamu Kimataifa katika tamasha la Filamu za Afrika hapa nchini Ujerumani Koloni." Alieleza Jazzphaa.

Ambapo alibainisha kuwa, filamu 97 kutoka nchi 25 za Afrika zinatarajiwa kuoneshwa kwenye tamasha hilo. 

Ikumbukwe kuwa, Mwaka 2016 mtengenezaji wa Filamu kutoka Tanzania Amil Shivji pia alipata nafasi ya kuchaguliwa kuonyesha Filamu yake ya Aisha. 

Aidha, Jazzphaa  aliwashukuru wadau wote kwa ushirikiano katika harakati zake mbalimbali ikiwemo ya kuongoza shughuli kwenye matamasha makubwa ya Kimataifa ikiwemo tamasha la Kimataifa la Filamu la nchi za Majahazi (ZIFF), Tamasha la Muziki la Sauti za Busara na mengine mengi pindi awapo Visiwani Zanzibar,  Tanzania. 

"Safari inaendelea. Asanteni wote mlionifanya kuwa na nguvu ya kuamini ninacho kifanya." Alimalizia Jazzphaa.

Tamasha hilo kwa mwaka huu ni la msimu wa 18  ambapo kila mwaka kimekuwa likipokea filamu mbalimbali kutoka Mataifa yote ya Afrika ambapo majaji uchagua zilizo bora na kuzipitisha.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.