Habari za Punde

VIJANA 300 WAPATA AJIRA ZA MUDA NGARAMTONI.

Baadhi ya vijana walichangamkia ajira za muda katika shamba la Soya linalomilikiwa na wakala wa mbegu bora za kilimo ASA kwenye eneo la Ngaramtoni wilaya ya arusha.
Mashine ya kuchambulia mbegu za Soya na kuwekwa kwenye mifuko maalum ya wakala wa mbegu bora za kilimo nchini.   

Na Lucas Raphael,Arusha

Zaidi ya wakazi 300 wa Ngaramtoni Wilaya ya Arusha mkoani Arusha wamechangamkia fursa ya Ajira zisizokuwa rasimi katika mashamba ya Wakala wa Mbegu za kilimo ASA yaliyopo mkoani humo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wakivuna Mbegu ya Soya wamesema uwepo wa mashamba ya Wakala wa Mbegu za kilimo umesaidia kupata Ajira kila siku tofauti na hapo awali hali ilivyo kuwa.

 

Wamesema Wakala huyo licha ya kutoa Ajira kwa jamii inayowazunguka wamekuwa wakipata elimu kubwa jinsi ya kulima mazao mbalimbali ikiwepo mahindi.

 

Nembwa Samweli mwenye umri wa miaka 45 alisema jamii inayozunguka mashamba ya ASA imekuwa ikinufaika kila msimu hususani wakati wa kuandaa mashamba,kilimo hasa kupanda kwa baadhi ya mazao pamoja na kupalilia sambamba na kuvuna.

 

Alisema kazi za Wakala wa Mbegu Bora za kilimo ASA nizakila wakati Hali iliyofanya kazi kiwepo kila siku nakufanya jamii iendelee kunufaika.

 

Frida Joram mwenye umri wa miaka 27 alisema Kama vijana wamepata eneo la kufanyia kazi nakujiongezea kipato tofauti na kukaa wakilalamika.

 

Alisema kwamba endapo vijana wakitumia fursa hiyo kwa malengo hawatoweza kukosa mitaji ya kufanya biashara kutokana na kuwepo sehemu yakupata fedha.

 

Alisema kuwa toka aanze kufanya kazi katika shamba hilo amekuwa na mabadiliko ya kiuchumi huku akiwataka vijana kuacha kuchagua kazi za kufanya.

 

Khalidi Athumani kijana mwenye umri wa miaka 30 alisema ana miezi mitatu akifanya kazi hiyo na tayari amekwisha anza kuona mabadiliko ya kiuchumi.

 

Mkuu wa shamba la Wakala wa Mbegu Bora za kilimo Ngaramtoni ,Mhandisi Lusia Wema  alisema jamii hiyo wamekuwa wakishirikiana nayo kwa nyakati tofauti ilikufanikisha azima nzima ya kilimo.

 

Alisema wakazi hao wamekuwa wakijitoa kufanya kazi mbalimbali za shamba kwa uaminifu mkubwa hali inayowafanya kuwa mabalozi wa zuri wa ASA.

 

Alisema licha ya kuwa wakazi hao hufanya kazi na kujipatia kipato lakini wamepata elimu juu ya kilimo Bora kinachozingatia vipimo kutoka kwa wataalam.

 

Mhindisi Lusia aliwataka vijana kutochagua kazi badala yake wafanye kazi zinazopatikana iliwapate kipato cha kujimu kimaisha tofauti na kukaa vijiweni ambapo wanaweza kujiingiza katika makundi ya vitendo vya kialifu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.