Habari za Punde

Wanawake Watakiwa Kuwa na Ushirikiano na Upendo.

Wanawake nchini wametakiwa kujenga upendo , mshikamano , huruma na kusaidiana wakati wanapopata matatizo.

Wito huo umetolewa na Katibu wa UWT wa Jimbo la Malindi Wilaya ya Mjini Unguja Bi.Mwanaidi Hassan juma wakati wa ziara yake katika Jimbo hilo kukaguwa waliokuwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi ambao kwa sasa ni wagonjwa ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha juma la Wanawake Duniani.

Amewataka kuacha kubaguana na kudharauliana na badala wake washirikiane katika kuendesha maisha yao ya kila siku ikiwemo kuwa na malezi ya pamoja na kupiga Vita udhalilishaji.

Adha amewataka wanawake kushiriki kwa wingi kugombania nafasi za uongozi ili kuweza kupata idadi kubwa ya wanawake watakaoweza kuwasilisha matatizo yao na kupatiwa ufumbuzi wa haraka.

Nao viongozi hao wameushukuru uongozi wa uwt kwa kuandaa ziara hiyo kwani imewapa moyo na kujuwa bado wanathaminiwa kutokana na mchango mkubwa walioutoa katika chama na taifa kwa ujumla.

Hata hivyo amewataka wanawake kuacha majungu,vitna,na uchochezi kwani Mambo hayo yanakwamisha kutekeleza mipango ya maendeleo waliojipangia.

Uongozi wa uwt Jimbo la malindi umefanya ziara kwa waliokuwa viongozi wa uwt ambao kwa sasa ni wagonjwa ukiwa Ni pamoja na Bi Nasra Mohd aliekuwa katibu wa chama Cha mapinduzi Jimbo la M/Mkongwe, Bi zahra moh'd aliekuwa katibu wa uwt tawi mchangani mjini,Bi mwatum Hilal aliekuwa sheha wa shehia ya Gulioni na Bi Salma Mselem aliekuwa Katibu wa UWT wilaya mjini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.