Habari za Punde

Bhaa atoa Michele na mafuta kwa madrsa 20 zinazosoma maulidi katika Jimbo lake.

Mwakilishi wa Jimbo la Mtoni Zanzibar Mhe Hussein Ibrahim Makuu (BHAA) amewataka Wazazi kushirikiana na Waalimu wa Madrasa ili kuwapatia elimu watoto wao na kurudisha maadili mema ya kizanzibar.

Mhe.Hussein Ibrahim Bhaa amesema maadili ya kizanzibari yanapotea kwa kiasi kikubwa hivyo iwapo watapata elimu itaweza kuwajengea na kuwa raia wema hapo baadae.

Ameyasema hayo huko Skuli ya Maandalizi na Msingi ya Sharifumsa wakati wa Utoaji wa mchele na mafuta kwa ajili  ya madrasa 20 zinazosoma Maulid ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) katika  Jimbo la Mtoni Zanzibar .

Amesema serikali inahitaji wataalamu wa fani mbalimbali Jambo ambalo litaiwezesha serikali kupata wataalamu na viongozi wema wa hapo baadae.

Amewataka wananchi kukumbushana na kuachana na hadaa za kidunia na badala yake wafanye Mambo mema kujenga akhera yao.

Kwa upande wake katibu wa Chama Cha mapinduzi wilaya ya mfenesini kesi mashaka ngusa amesema juhudi zinazochukuliwa na viongozi wa Jimbo la mtoni ni kubwa na kuwaomba wanachi kushirikiana ili juhudi hizo zizidi kuimarika.

Hata hivyo amewaomba wananchi kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na viongozi wao ili malengo yaliokusudiwa yaweze kufikiwa.

Nao baadhi ya waalimu wa madrsa zilizokabidhiwa msaada huo wamesem msaada huo imekuja kwa wakati muafaka kwani utasaidia kusoma maulidi yao bila usumbufu na kuwaomba viongozi wengine kuiga mfano wa kiongozi huyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.