Habari za Punde

Dr Shein aongoza kikao cha kamati maalum ya CCM Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Bi. Lela Burhani Ngozi, alipowasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar kuhudhuria Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichofanyika leo 18-10-2021.Picha na Ikulu)
WAJUMBE wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar wakiwa katika ukumbi wa mkutano Afisi Kuu ya CCM Zanzibar, wakipitia makabrasha kabla ya kuaza kwa Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar, kilichofanyika leo kilichoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi  Zanzibar Rais Mstaaf wa Zanzibar Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein.
WAJUMBE wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar  wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi  Zanzibar Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) akiongoza Kikao cha Kamati Maalum ya CCM Zanzibar kilichofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.  
 MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein akiongoza Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar, kilichofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar na (kulia kwake) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe Hemed Suleiman Abdulla.
(Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.