Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akizungumza na watendaji wa Mkoa wa Singida wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati ya Mawaziri 8 wa Kisekta yenye lengo la kutatua migogoro ya ardhi walipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida leo.
Na Happiness Shayo- WMU
Watendaji wa Mikoa, Wilaya, Miji na Vijiji nchini
wametakiwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kuhakikisha wanasimamia vizuri maeneo
ya hifadhi ili kuepusha migogoro kati ya wananchi na Serikali.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii Mhe. Mary Masanja (Mb) alipokuwa akizungumza na watendaji wa mkoa wa
Singida katika kikao cha Mawaziri 8 chenye lengo la kutatua migogoro ya ardhi
kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida leo.
“Migogoro ya wananchi kuvamia maeneo ya hifadhi
inajitokeza wakati watendaji wenye dhamana na walioajiriwa na Serikali wapo
wanatazama tu mpaka inafikia katika hali hii” Mhe. Masanja amefafanua.
Mhe. Masanja ameongeza kuwa mtendaji yeyote
atakayehusika katika kusababisha migogoro ya wananchi kwa kutosimamia vizuri
eneo lake la kazi hastahili kwenda na kasi ya awamu ya sita na ana mpango wa
kurudisha nyuma jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia
Suluhu Hassan za kutatua migogoro.
“Hakikisheni kwamba maeneo yote ya hifadhi ambayo
tunayaachia kwa ajili ya wananchi mnayasimamia vizuri ili kumpa nafasi Mhe.
Rais kutekeleza majukumu yake vizuri ya kuwahudumia wananchi.
Ameongeza kuwa migogoro hiyo ambayo Mhe. Rais Samia
Suluhu Hassan ameisimamia na kutoa suluhu yake kwa kuiagiza Kamati ya Mawaziri
8 wa Kisekta kuitatua si vyema ikajirudia.
No comments:
Post a Comment