Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said amefanya ziara katika Chuo cha Mafunzo ya Amali cha NORTH ATLANTIC cha Qatar na kufanya mazungumzo na Rais wa Chuo hicho, Dr Salem Al-Naemi.
Katika mazungumzo yao, wamekubaliana kujenga mashirikiano ya kielimu kwa ajili ya wanafunzi wa Zanzibar.
Mazungumzo hayo yataendelezwa kupitia Wizara ya Elimu pamoja na Ubalozi wa Tanzania.
Chuo hicho kinafundisha fani mbalimbali zikiwemo ufundi na uhandisi.
No comments:
Post a Comment