Habari za Punde

Kumsaidia Dada Mishal Sumary Kwenda Kutibiwa Nchini India.


Anaandika Malisa GJ 

Usiku wa December 26 mwaka 2011 (boxing day) siku ambayo Wakristo hufungua mabox ya zawadi za Christmas, dada Mishaly Sumary alifungua box la maumivu yaliyompa ulemavu wa kudumu. Alikua anatoka Burere Hospital (kwa Dr.Bake) Kibaha alipokua anafanya kazi kama muuguzi.

Katikati ya giza aliona vijana watatu wakimfuata lakini hakuwa na wasiwasi. Aliamini ni watu wanaendelea na shughuli zao tu. Lakini ghafla walimvamia na kumshambulia kwa marungu na nondo.

Walimvunja mkono, wakamvunja mguu, wakavunja nyonga, wakavunja taya, wakamng'oa meno, wakamtegua shingo na kumvunja uti wa mgongo. Alipoteza fahamu na kuzinduka akiwa kitandani MOI.

Hakujua kwanini watu wale walimfanyia ukatili huo kwa sababu hajawahi kuwa na "bifu" na mtu. Ilimuumiza sana. Kilichoumiza zaidi ni kuwa polisi hawakukamata mtu yeyote kuhusika na tukio hilo. Hadi leo imebaki kuwa "watu wasiojulikana"

MOI walijitahidi sana kumpa matibabu. Walifanikiwa kuunga mguu, wakaunga mkono, wakaunga nyonga, wakaunga shingo (japo bado anatumia neck support), wakaunga taya (japo midomo ya juu na chini imepishana kidogo), pia wakampatia meno bandia kufidia yale yaliyong'olewa na wale wauaji.

Lakini hawakufanikiwa kuunga uti wa mgongo. Wakamuandikia rufaa kwenda India. Ktokana na hali ngumu kiuchumi hakuweza kwenda India. Dada Mishally alilala kitandani kwa miaka minne hadi 2014 alipopata mfadhili aliyempeleka India. Lakini bahati mbaya fedha ziliisha kabla hajakamilisha matibabu. Hivyo akalazimika kurudi.

Kwa kipindi chote toka aliporudi mwaka 2014 hadi sasa bado yupo kitandani. Hii ina maana kuwa ametimiza miaka 10 kwa kulala tu kitandani. Ni Miaka 10 ya mateso, maumivu, shida na karaha.

Jiulize ukiugua malaria ukalala kitandani siku mbili unakua kwenye hali gani? Halafu vuta picha mtu aliyelala kitandani miaka 10. Na sio kwamba alizaliwa hivyo. Hapana. Ni wanadamu katili wamemsababishia. Alizaliwa mzima, na akasoma hadi kuwa muuguzi. Alikua na ndoto zake nyingi maishani lakini wahuni wachache wakaamua kuharibu maisha yake. Inauma sana 😭.

Kutokana na kulala muda mrefu amepata vidonda vingi mgongoni (bedsores) na pia amepata changamoto kwenye mfumo wake wa uzazi.

Nimemfahamu dada Mishally tangu mwezi July mwaka jana 2020 kupitia wanafamilia wawili wa Gifted Hearts ambao walikua wakimsaidia mahitaji madogo madogo kwa kipindi kirefu. Hao ndio walioniunganisha na dada Mishally.

Tulipokutana aliomba msaada wa kurudi India kumalizia matibabu, kwa sababu walimhakikishia kuwa anaweza kutembea tena.

Hata hivyo tulishindwa kumsaidia kipindi hicho kwa sababu tulikua na wagonjwa watano India waliokua wanatutegemea kwa kila kitu. Hivyo kuongeza mwingine ingetuwia vigumu kuwahudumia wote kwa wakati mmoja. Tukamuomba asubiri angalau wapungue.

Wakati akisubiri, tuliamua kumsaidia mahitaji yake ya muhimu. Mimi na marafiki zangu 7 tukajichanga na kumlipia kodi ya nyumba ya mwaka mzima. Na tukajiwekea utaratibu wa kumtembelea kila mwezi na kumpelekea mahitaji muhimu kama chakula, pampas, umeme, maji etc.

Kwa sasa angalau idadi ya wagonjwa waliopo India imepungua kidogo. Wamebaki wawili, hivyo dada Mishally anaweza kusaidika, maana ameshasubiri zaidi ya mwaka mmoja.

Amepata nafasi hospitali ya Appolo, New Delhi. Gharama za upasuaji, clinic na ppstmedication care kwa miezi mitatu atakayokaa huko ni $43,000 sawa na TZS 90M. Kwahiyo ukijumlisha nauli (yake na atakayemsindikiza), pamoja na gharama za kuishi India kwa miezi miatu ya matibabu, zinaweza kufika 100M.

Kwa kuwa gharama hizi ni kubwa tumezungumza na menejimenti ya hospitali ili angalau tujichange zikitimia 40M Mishaly atangulie India kwa matibabu halafu tuendelee kuchanga akiwa huko.

Hivyo basi tutakua na challenge ya saa 72 za kurudisha tabasamu kwa dada Mishally kwa kutafuta 40M za kuanzia matibabu, halafu nyingine tutachanga akiwa tayari India.

Fedha zote zinapokelewa na Mishaly mwenyewe kupitia M-Pesa 0766180656, Tigopesa 0718626642 au Bank Account (CRDB ) 0152078706601, jina Mishaly Sumary.

Asante sana na Mungu akubariki.! 🙏🏾

#GiftedHeart #RudishaTabasamu #LetLoveLead #MalisaGJ

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.