Habari za Punde

Asilimia 17 ya Watoto Wachanga Wanazaliwa na Uzito Mdogo ( Njiti) Tanzania.

Daktari bingwa wa Watoto katika Hospitali ya Bombo Tanga Mohamed Swalehe akifafanua jambo mbele ya Kaimu Katibu Tawala Ndg.Noel Kazimoto  (kushoto) na (kulia) Afisa Mfawidhi wa hospitali hiyo Bi.Naima Zacharia, wakati alipotembelea Hospitali hiyo.
Kaimu Katibu Tawala Mkoani Tanga Ndg.Noel Kazimoto akiwa katika picha ya pamoja na Wauguzi wa wodi ya watoto njiti katika hospitali ya Rufaa ya Bombo jijini Tanga.
Kaimu Katibu Tawala Mkoani Tanga Ndg.Noel Kazimoto akiongea wakati wa maadhimisho hayo.
Kaimu Katibu Tawala Ndg. Noel Kazimoto akimkabidhi zawadi Ndg.Willium Juma mkazi wa Tanga jiji ambaye mke wake alijifungua watoto njiti mapacha watatu na kuhudumiwa katika hospitali hiyo.


Na Hamida Kamchalla, TANGA.

TANZANIA imetajwa kuwa ni miongoni mwa nchi ambazo zinakabiliwa na vifo vya watoto wachanga chini ya mwezi mmoja ambapo idadi kubwa  ikiwa ni watoto njiti, huku takwimu zikionesha kati ya asilimia 13 hadi 17 ya watoto wanaozaliwa nchini ni watoto njiti.

Hayo yalisemwa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Ndg.Noel Kazimoto wakati akizungumza katika kongamano la kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto njiti duniani liliyofanyika katika viwanja vya Hospitali ya rufaa Bombo jijini Tanga.

Kazimoto alisema tatizo hilo la vifo vya watoto wachanga  linasababishwa na magonjwa mbalimbali yanayo wakabili wakina mama wakati wa ujauzito na kutaja kuwa ni pamoja na unywaji wa dawa kiholela bila kufuata maelekezo ya daktari.

"Kati ya asilimia 13 hadi 17 ya watoto wote wanaozaliwa nchini wanazaliwa wakiwa njiti, tatizo hili husababishwa na sababu mbalimbali za magonjwa zinazowapata wakina mama  wakati wa ujauzito zikiwemo, shinikizo la damu, sukari, lishe hafifu, lakini pia sababu za kimaumbile kwenye mfumo wa uzazi pamoja na watoto kuzaliwa zaidi ya mmoja" alisema.

Aidha Kazimoto alisema serikali ya awamu ya sita imekua ikifanya jitihada mbambali katika kuhakikisha inaboresha huduma zilizo bora za afya kupitia fedha za UVIKO 19 hususani katika kuboresha huduma za mama na mtoto na pia kuwashukuru madaktari na wahuguzi kwa jitihada mbambali wanazozifanya katika kusaidia utoaji wa huduma kwa wananchi.

"Watoto wanaozaliwa kabla ya miezi 9 wenye uzito mdogo huhitaji huduma za uangalizi zikiwemo matibabu na lishe mpaka watakapotimiza umri wa mwaka mmoja, kulea mtoto wa aina hii ni kazi ngumu sana, nimeambiwa hapa pana madaktari bingwa wanaofanya kazi ya kulea hawa watoto, hongereni sana kwa jitihada zenu za kuhakikisha wanakua vizuri" 3aliongeza.

Akisoma taarifa kwa mgeni rasmi Mganga Mfawidhi Hospitali ya Mkoa Dkt. Naima Zacharia alisema wapo watoto 10 ambao wamezaliwa njiti huku mwenye uzito mdogo zaidi akiwa na uzito wa gramu 700 ambapo pamoja na mafanikio hayo hospitali ianakabiliwa na changamoto ya vifaa vya matibabu.

"Wapo watoto kumi waliozaliwa na uzito mdogo, ambaye mwenye uzito wa chini sana alikuwa na gramu 700, hospitali hususani wodi ya watoto njiti inakabiliwa na uhaba wa vifaatiba vinavyosaidia watoto njiti kupumua, vifaa vya kupatoa joto, vifaa vya kuonelea manjano pamoka na vifaatiba vingine" alieleza.

Baadhi ya wazazi wenye watoto njiti wameelezea ugumu wa malezi ya watoto wa aina hiyo kuwa ni mgumu kwani hata kuwashika inakuwa tabu kutokana na maumbo yao yalivyokuwa madogo huku wakiwashukuru madaktari na wauguzi kwa kuwapatia huduma zilizo bora na pia kuwataka wazazi  wenye watoto njiti kutokata tamaa katika kuwalea watoto wao.

"Mimi mtoto wangu nilimzaa na gramu 750 kalikuwa ni kadogo sana kuliko wote nilikuwa naogopa hata kumshika huyu mtoto, wanawake wenzangu naomba msife moyo mtoto njitu anaishi hasa uki.lea kwa mapenzi, ila nawashukuru sana madaktari wote ambao wanalea watoto njiti" alibainisha Maria Joackim.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.