Habari za Punde

Meya wa Jiji awaagiza madiwani kusaidia kurejesha watoto waliotoroka skuli


Na Maulid Yussuf, Wema 

Meya wa jiji la Zanzibar Mhe. Mahmoud Mohammed Mussa amewataka Madiwani kutumia nafasi waliyonayo kwa kuwarejesha watoto waliotoroka Skuli ili kuepuka kukosa wataalamu wa hapo baadae.

Akifungua mkutano wa Madiwani wa Mkoa wa Mjini Maghribi juu ya kuwapa uelewa wa mradi wa kuwarejesha watoto Skuli amesma hatua hiyo ni katika harakati za kuhakikisha wanatimiza ilani ya Chama cha Mapinduzi, kwa kushirikiana na jamii kuona hatua ya kuwarejeaha watoto skuli inafikiwa.
Amewataka kuhakikisha watoto walioacha skuli wanarudi ili kuisaidi Taifa kupata wtalmu zaidi na kuepusha kupata watoto chokoraa ambao wanaweza kuilete aif mbaya Taifa.
Amesema idadi ya watoto waliotoroka inaonekana ni kubwa na inatishia kukosa Taifa bora, hivyo ni vyen kushirikin ili kuhkikisha mradi huo unafikiwa.
Nae Mjurugenzi idara ya Mipango sera na Utafiti Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zazibar bwana Khalid Masoud Waziri amesema utafiti wa idadi ya watoto hao umefanywa mwaka 2018, hivyo UNICEF umeona umuhimu wa kuongeza nguvu ili kuhkikisha wtoto hao wanarudi Skuli.
Akiwasilisha mada juu ya mradi wa kuwarejesha watoto Skuli, Mratibu wa mradi huo bwana Mzee Shirazi amesema wapo walimu ambao wanakuwa na lugha mbaya kwa watoto wanaorejea Skuli kwa kuwabeza kutokana na kutoroka kwao.
Amewataka Madiwani kuhakikisha wanafanya kazi vizuri kwa kushirikiana na kuwafichua Walimu wenye tabia hiyo ili kuona malengo yayokusudiwa yaweze kufikiwa.
Wakitoa michango yao Madiwani hao wamesema, viingozi wana dhima kubwa kwa jamii katika kuona maendeleo yanafikiwa katika nyanja mbalimbali, hivyo ni wajibu kwao kuhakikisha malengo yaliyowekwa Serikali yanafikiwa.
Wamesema kuna tatizo la watoto wenye ulemavu wa aina mbalimbali nao miongoni mwa watoto wanaotoroka Skuli, hivyo ni lazima kuhakikisha wanawajengea mazingira rafiki ili waweze kusoma pamoja na kuwasaidia watoto waliodhalilishwa kwani wanaonekana pia kuacha Skuli.
Hata hivyo wameshuri kuwatumia wrtibu wa dwati wa jinsia wanwke n wtoto waliopo katika shehia mbalinbali kwani nao wana nafasi kubwa ya kuwatambua watoto hao na kusaidia kuwrejwsh wtoto hao.
Jumla ya watoto 35732 wanatarajiwa kurejeshwa Skuli kwa Zanzibar kutokana na kutoroka kwa sababu mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.