Na Kassim Abdi, OMPR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abbdulla aliupongeza uongozi wa Bugema University kutoka Uganda kwa kuja kuwaona wanafunzi waliojeruhiwa kufuatia ajali ya basi iliotokea Mkoani Shinyanga Juni 02 Mwaka huu.
Mhe. Hemed alieleza hayo wakati alipofanya mazungumzo na uongozi wa chuo hicho uliofika ofisini kwake vuga kwa ajili ya kujitambulisha na kubadilishana mawazo kuhusina na masuala mbali mbali ya kitaaluma
Alisema kuwa, serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia wizara ya afya inaendelea kuwahudumia kwa karibu wale wote waliopata ajali iliosababisha majeraha na wengine kupoteza viungo ili kuimarisha Afya zao.
Alifafanua kuwa, Serikali itaendelea kuwahudumia wahanga hao kwa lengo la kuziimirisha Afya zao ili waendelee na majukumu yao katika kulitumikia taifa.
Aidha, Makamu wa Pili wa Rais aliuhakikishia uongozi wa BUGEMA UNIVERSITY kwamba serikali zote mbili zitaendelea kushirikiana na chuo hicho katika kuhakikisha azma iliokusudiwa ya kuwataarisha wanafunzi kuwa wataalamu bora kupitia kada ya Afya iweze kufikiwa.
Nae Makamu Mkuu wa chuo hicho Prof. PAUL KATAMBA alimueleza Makamu wa Pili wa Rais kuwa, uongozi wa chuo umeamua kuja Zanzibar kwa lengo la kuziona na kuzifariji famila za wahanga pamoja na familia za wafiwa.
Pia Prof KATAMBA alisema kuwa kufuatia wahanga wa ajali waliopo Zanzibar kwa sasa chuo kimeamuwa kuja na utaratibu maalum wa masomo kwa kutumia njia ya mtandao (Online Study), njia ambayo itawawezesha wanafunzi hao kumalizia masomo yao wakiwa zanzibar.
No comments:
Post a Comment