Habari za Punde

Familia ya Bw. Ahmed Khamis (Mcheju ) Yatowa Pongezi Kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.


*Bismillahi Rahmanir Rahiim*

Kwa heshima taadhima na unyenyekevu nichukue fursa hii kwa niaba ya familia ya Bwana Ahmed Khamis (Mcheju),kumpongeza na kumtakia kheri na salama Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk.Hussein Ali Mwinyi kwa kutimiza Mwaka mmoja wa Uongozi wa kuiongoza Zanzibar, 

*Kwa Hakika kama familia tunaridhika mno na Uongozi wake* na tunazidi kumuombea Dua kwa Mwenyezi Mungu,muumba wa Mbingu na Ardhi ampe wepesi katika Majukumu yake mazito.

*Tunamtakia kheri na Salama yeye na familia yake.*

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.