Na
Saadam Seif - Arkuu
Katibu
Mkuu anaeshuhulikia masuala ya Uchumi na Uwekezaji Afisi Ya Rais
Kazi Uchumi Na Uwekezaji Habiba Hassan Omar amesema serikali ina mpango
wa kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi kutika kuandaa miji yenye ubora na
urahisi wa shughuli mbali mbali.
Ameyasema
hao afisini kwake Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharib B wakati akizungumza
na wataalamu wa kampuni ya Crm Land Consultant Ltd kwa lengo
la kujadiliana juu ya kuandaa mpango kabambe wa matumizi bora ya ardhi katika
eneo la uwekezaji Fumba (Master Plan)
Katibu
Habiba amesema ni mapendekezo ambayo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeyapokea
na imedhamiri kulifanyia kazi suala hilo na itahakikisha inabadilishina maoni
na wadau mbali mbali wa masuala hayo ili kuona kwa namna gani mpango huo
unafanikiwa katika utekelezaji wake.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Crm Land Consultant Ltd Dk
Clara kweka amesema lengo la kuzungumza pamoja na katibu huyo kutawasaidia
kuandaa vyema mpango huo ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa katika mpango wa
serikali wa kuandaa mipango miji.
No comments:
Post a Comment