Habari za Punde

Uongozi wa Chuo Kikuu cha Postdam kutoka Ujerumani ziarani Manispaa ya Mjini

Raisi wa Chuo kikuu cha Postdam  Prof. Oliver Gunther alipofika alipokuwa akitembelea Bustani ya Botanic Migombani  ili kujione jinsi mabadiliko ya tabia nchi yanavyoathiri 
Raisi wa Chuo kikuu cha Postdam  Prof. Oliver Gunther alipofika alipokuwa akitembelea Bustani ya Botanic Migombani  ili kujione jinsi mabadiliko ya tabia nchi yanavyoathiri 
Katibu Jumuiya ya Uhifadhi wa Mazingira Mnara Mbao Kombo Juma Maalim akisoma risala wakati walipotembelewa na Rais wa chuo kikuu cha Postdam na ujio wake katika Bustani ya Botanic iliopo Migombani Mjini Unguja .

Raisi wa Chuo kikuu cha Postdam  Prof. Oliver Gunther akizungumza na jumuiya ya Uhifadhi wa Mazingira Mnara wa Mbao mara alipofika katika Bustani ya Botanic na ujio wake kutembelea.


Uongozi wa Chuo cha Postdam kutoka Ujerumani wakiwa katika picha ya pamoja na wasimamizi wa Bustgani ya Botanic walipofika kuitembelea.
PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR 

Rais wa Chuo Kikuu cha Postdam  kutoka Ujeruman  Proff. Oliver Gunther  amesema mashirikiano yaliopo na Manispaa ya  Mjini yatasaidia kuhifadhi na kudhibiti mazingira ya Bustani ya Botanic Migombani  ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia Nchi.


Aliyasema hayo wakati wa ziara yake akiwa na ujumbe aliyofuatana nao  alipotembelea katika bustani hiyo na  kuangalia uhifadhi wa mazingira na kupata fursa ya kupanda miti mbalimbali ya kiasili ikiwemo miti iliopotea katika bustani hiyo.


Amesema uhifadhi wa miti husaidia kuimarisha mazingira pamoja na kuthibiti wanyama  wengi wasipotee jambo ambalo huipendezesha na kuipa haiba bustani hiyo.


Nae Mstahiki Meya wa Zanzibar Ali Haji Haji amesema amefurahishwa na ugeni ulowafikia kutoka Postdam Ujerumani ambao ni  marafiki wao wa muda mrefu takribani miaka 10 ,kwa kutunza na kuhifadhi mazingira ya bustani hiyo pamoja na kufanya tafiti mbalimbali za miti ya kiasili.


Aidha amesema matarajio yao kutokana na ugeni huo ni kuongeza mashirikiano ya pamoja katika kuinyanyua bustani hiyo na kuirejesha miti ya asili ambayo imekwisha toweka,


Nae Mkurugenzi wa Manispaa ya Mjini Ali Khamis Mohammed amefahamisha kuwa  Chuo kikuu cha Postdam Ujerumani  hutoa misaada mbali mbali ya kuimarisha bustani hiyo kwa lengo la kuirejesha hadhi yake ya awali .


Aidha alieleza Manispaa ya Mjini itaendeleza kushirikiana na wadau ili kuimarisha bustani mbali mbali zilizopo katika Manispaa hiyo,


Kwa upande wa Mkuu wa Idara ya Huduma za Jamii na Mazingira, Manispaa ya Mjini Mwanajuma Ali Abuod ameutaka Ujumbe huo kuitumia fursa hiyo kwa kufanya tafiti za kisaikolojia ya miti katika Manispaa ya Zanzibar .


“Muitumie fursa muliyoipata kwa kufanya tafiti zenu za kisaikolojia ya miti itasaidia zaidi  kuitangaza Zanzibar ,’’alisema Mkuu huyo.


Alisema Ujio wa Ugeni huo utasaidia kuengeza mashirikiano kwa kubadilishana mawazo na kujifunza taaluma iliopo katika bustani ya botanic.


Nae Katibu wa Jumuiya ya Hifadhi ya Mazingira Mnara wa Mbao Kombo Juma Maalimu akieleza changamoto zilizopo ikiwemo ukosefu wa vitendea kazi , pamoja na mafunzo ya kiutaalamu ya uendeshaji wa bustani hiyo.


Vile vile alisema ukamilishwaji wa bwawa la kufugia samaki na pembea za kuchezea watoto pamoja na kukiomba Chuo Kikuu cha Postdam  kuingiza Bustani ya Migombani (Botanic Garde) na  ziliopo duniani ili ipatikane fursa za kimasomo na kubadilishana uzoefu .  

 

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.