Habari za Punde

Uwepo wa Bandari ya Tanga ni Chachu ya Maendeleo ya Uchumi wa Taifa.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.Adamu Malima akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kukabidhiwa vifaa vya kutendea kazi baharini.
Mkuu wa Mkoa akiwa na viongozi mbalimbali wa Mkoa katika ukaguzi wa bandari ya Tanga
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adamu Malima akiongea kuhusu maendeleo ya bandari ya Tanga mbele ya waandishi wa habari, kishoto kwake ni Meneja wa Bandari mkoani Tanga Mhandisi Donald Ngaire.

Na Hamida Kamchalla, TANGA.

SERIKALI mkoani Tanga imesema ujenzi wa bandari kavu iliyojengwa eneo la Malula, mkoani Arusha itasaidia kupunguza shehena za mizigo kwa haraka kwenye bandari ya Tanga na kusaidia kulinda miundombinu ya barabara kwa muda mrefu.

Hayo yalibainishwa na mkuu wa Mkoa wa Tanga Adamu Malima wakati akipokea mrejesho wa kikao cha kutangaza maendeleo ya Mkoa huo kilichafanyika hivi karibuni jijini Arusha sambamba na kupokea vifaa vya kufanyia kazi bandari ya Tanga.

Vifaa vilivyoingia bandarini hapo ni boti moja ya kuongozea meli pamoja na vifaa mashine kubwa tatu za kupakulia makontena ya mizigo kuingiza na kutoa kwenye meli ambavyo vimeletwa na Mamlaka ya Bandari nchini na kukabidhiwa kwa mkuu wa Mkoa.

"Tunahitaji tuwe na sehemu ya kupumulia, kwahiyo jambo la kwanza tumahitaji reli ile iingie mpaka bandarini, halafu tunaitaka hiyo reli yenyewe itoke nje sasa iende mpaka Arusha kwenye eneo letu la bandari ya nchi kavu" alisema Malima.

"Pale sasa inakuwa hii mizigo yote ambayo inakuja Tanga ikifika tu pale inabebwa mara moja baada ya masaa nane unapakua mzigo wako, baada ya masaa nanw unachukua mzigo wako Arusha unakwenda zako, jambo jingine ambalo ni kubwa zaidi ni kwamba itaondoa magari, tunaweka magari ya tani 40 yanakuwa karibu 100, kila siku unaweka magari yanakuja hapa yanaharibu barabara, sasa yataishia kule Arusha" aliongeza.

Aidha Malima alisema kuwa wamedhamiria kuifanya bandari ya Tanga kuwa bandari ya pekee kisafirisha bidhaa zote zinazotokana na zao la mkonge kwasababu Tanga ni mkonge na mkonge ni Tanga huku akisema wana mpango wa kuendelea kuwavutia na kuhamasisha wateja wao kutumia bandari hiyo.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Bandari mkoani Tanga Donald Ngaire alisema wadau wameunga mkono ujenzi wa bandari kavu kwakuwa itawapunguzia garama za usafirishaji ambapo ikizingatiwa kupanda kwa hali ya kiuchumi lakini pia itakuwa ni fursa nyingine kwa wananchi katika kipindi chote cha ujenzi huo.

"Wadau wengi tulipokuwa kule Arusha wameonyesha nia ya kusema kwamba ni faraja kwao kama bandari itakengwa katika eneo la malula kwasababu kwanza itawapunguzia garama za kusafiri moja kwa moja kutoka Arusha hadi hapa Tanga" alisema Ngaire.

Aidha Ngaire alisema kuhusu vifaa vilivyoletwa bandari ya Tanga vitaongeza ufanisi lakini pia muda wa meli kukaa bandarini utapungua ikiwa ni sambamba na kuvutia wateja kibiashara ili kuongeza tija na utendaji jambo litakalopelekea bandari hiyo kuongeza uzalishaji kwa upande wa usafirishaji.

"Lakini cha msingi zaidi ni kwamba uwepo wa vifaa hivi vya kutendea kazi vitavutia biashara, anapokuja mteja halafu anakuta vifaa ni vichache kunamsumbua kwahiyo anapokuta vifaa maana yake itamvutia na watu wengi watapenda kupitishia mizigo hapa Tanga" alifafanua Ngaire.

Aidha alitoa wito kwa wananchi kutumia bandari ya Tanga ambayo kwa sasa maboresho yake ni kiasi kikubwa katika kutoa huduma kwa wateja wake, "kutoa msukumo kwa wafanyabiashara kuweza kuitumia bandari ya Tanga kwa vile imeboreshwa kwa kiwango kikubwa lakini pia italeta maendeleo ya haraka na kurahisisha biashara miongoni mwa wananchi".

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.