Habari za Punde

Jamii Yatakiwa Kutenga Muda Kwa Ajili ya Mazoezi ya Viungo - Mhe Hemed.

Na.Abdulrahim Khamis.OMPR.

Jamii imetakiwa kutenga muda kwa ajili ya kufanya mazoezi, ili kuujenga mwili kuwa na Afya bora.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla alitoa wito huo alipojumuika pamoja katika mazoezi na wanavikundi vya mazoezi Zone “A”  katika uwanja wa Maisara jijini Zanzibar.

Mhe. Hemed alielezea kufurahishwa kwake kwa kuona muako wa wazanzibari katika kufanya mazoezi kuwa mkubwa jambo ambalo litasaidia kupunguza wagonjwa wa maradhi mbali mbali ikiwemo presha na kisukari.

Aliwataka wananchi kutenga muda maalum wa kufanya mazoezi kwa ajili ya kuushughulisha mwili ili kuichangamsha akili na kuepukana na athari zisizokuwa za lazima.

Alisema ni jambo la kufurahisha kuona makundi ya Rika mbali mbali, ikiwemo vijana, watu wazima na kina mama kutenga muda wao kwa kushiriki mazoezi hayo, jambo ambalo linaleta faraja kuwa jamii imefahamu umuhimu wa kufanya mazoezi kila siku.

Sambamba na hayo Mhe. Hemed alisema serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na Rais Dr Mwinyi imedhamiria kuleta hamasa katika michezo, ikiwemo suala la mazoezi ya viungo,  hivyo ni vyema kwa wanamichezo hao kutumia fursa hiyo kuweza kujiendeleza zaidi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha wafanya mazoezi ya viungo Zanzibar Said Suleiman Said alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa

Nae, katibu wa ZABESA Suleiman Yussuf Sitwale alieleza kuwa Zone A ina jumla ya vikundi 12 ambapo inajumuisha vikundi vilivyopo kuanzia Serena hadi mazizini, ambapo wamemuomba Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa mlezi wa Ukanda huo.

Alileza kuwa, Mazoezi hayo ni matayarisho ya siku ya mazoezi ya viungo Januari 01 ya kila mwaka ambapo kwa mwaka huu wanategemea kupokea wageni zaidi ya 400 kutota Tanzania bara.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alianza mazoezi kwa kutembea kutoka nyumbani kwake mazizin, kushukia mnazi mmoja, kikwajuni na kumalizia uwanja wa Maisara.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.