Habari za Punde

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania Atembelea Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Chamwino Dodoma.

 


Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji John Masunga, akifanya ukaguzi wa hatua za mwisho za Ujenzi wa Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Chamwino, Dodoma leo tarehe 24 Desemba, 2021 ambacho kinategemewa kuzinduliwa mapema Mwezi Januari, 2022.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji John Masunga, leo 24 Desemba, 2021 amefanya ukaguzi wa mradi wa Ujenzi wa Kituo Cha Zimamoto na Uokoaji unaoendelea katika Wilaya ya Chamwino, jijini Dodoma.

Ujenzi wa kituo hiki unafanywa kwa kutumia akaunti ya nguvu kazi “Force account” ukisimamiwa na kuratibiwa na wataalamu wa Ujenzi wa ndani wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Ujenzi wa kituo hiki umegharimu   jumla ya Shilingi bilioni moja na milioni mia mbili, fedha ambazo zimetoka Serikali kuu. Ujenzi wa kituo hiki umekamilika kwa asilimia mia moja na kituo kinakusudiwa kuhudumia wakazi wa Wilaya ya Chamwino pamoja na wakazi wa maeneo jirani.

Kamishna Jenerali aliwapongeza waratibu wa ujenzi wa kituo hiko na kusema

“Nawapongeza sana waratibu wa mradi huu kwa kuhakikisha mradi huu unakamilika kwa wakati aidha niwatake kuongeza kasi zaidi kukamilisha sehemu ambazo zimebakia kwani tunatarajia kituo hiki kitazindulliwa mapema Mwezi Januari, 2022”

Katika ziara hiyo, Kamishna Jenerali aliambatana na Viongozi Waandamizi wa Jeshi hilo ambao kwa pamoja wameridhishwa namna mradi unavyoendelea.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.