Habari za Punde

Taifa Cup 2021 Music Challenge Yamalizika Kwa Mikoa Kutoa Mastaa Wapya

Washindi wa Muziki wa kizazi kipya walioibuka ushindi wa Tatu Asma Athuman na Asnath Athuman kutoka Mkoa wa Dar es Salaam, wakikabidhiwa zawadi yao.

Na Mwandishi Wetu

“Ngoja niseme hili najua wapo ambao hawatanielewa, kwa jinsi unavyoimba na kukaa kwenye key hakuna msanii yeyote katika ‘top five’ ya sasa ya Bongofleva anayeweza kukufikia,” ni kauli ya mtu ambaye kwa miaka 28 mikono yake imetengeneza baadhi ya “biti” kali na za kihistoria za muziki nchini mtayarishaji mkongwe ambaye masikio yake yamesikia sauti nyingi za wasanii waliotoka wakawa maarufu kuliko na walioishia studio, si mwingine bali ni P’ Funky.

Hiyo ni kauli inayoweza kuonesha vipaji ambavyo nchi hii inavyo kitaa na jana vilipata fursa kuonekana kwenye platform kubwa iliyoandaliwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Taifa Cup Music Challenge.

Kwa upande wa Bongofleva wasanii 10 waliowakilisha mikoa yao walingia fainali na kwa upande wa Singlei wasanii wanne waliingia fainali kusaka washindi watatu. Matokeo yakawa hivi kwa jina na mkoa husika: 
Washindi wa Singeli: 
 
1st  Hamza  Juma  Hamza - Morogoro
2nd Abdulkadri Mwana  Kwangaya- Dsm
3rd  Saleh Abas Zuber - Mjini Magharibi

*Muziki wa kizazi kipya: *

1st  Abisai Kassanga - Pwani
2nd Meshack Ngemela- Mbeya
3rd Asma Athuman na Asnath Athuman- DSm. _

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.