Habari za Punde

WAZIRI UMMY: TUTAWASHUSHA VYEO WALIMU WAKUU WATAKAOCHANGISHA MICHANGO ISIYOFUATA UTARATIBU

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Ummy Mwalimu akizungumza leo mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea ujenzi wa Madarasa mapya katika shule ya Sekondari Saruji Jijini Tanga kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa
Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Ummy Mwalimu aliyesimama kulia ya kukagua Ujenzi wa Madarasa katika Shule ya Sekondari saruji Jijini Tanga.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Ummy Mwalimu katika akisisitiza jambo kwa Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa kulia wakati wa ziara hiyo kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Maweni
NA OSCAR ASSENGA, TANGA.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Ummy Mwalimu ametoa onyo kali kwa walimu wakuu wa shule za Msingi na Sekondari kuacha kuchangisha michango isiyofuata utaratibu na watakaobainika kufanya hivyo watachukuliwa hatua kali ikiwemo kushushwa vyeo.

Ummy alisema hayo leo wakati wa ziara yake Jijini Tanga ya kutembelea ujenzi wa madarasa 14 katika shule ya Sekondari ya Saruji iliyopo Jijini Tanga iliyojengwa na fedha za Uviko 19 wenye thamani ya Sh.Milioni 280 huku akiridhishwa na ujenzi huo.

Alisema kwamba kwa sekondari wanasisitiza viondolewe vikwazo kwa watoto wanaoanza kidato cha kwanza lakini michango isiyofuata utaratibu tutalala mbele na walimu wakuu na hatanii.

“Niwaambie kwamba katika hili sitanii tumeshashusha vyeo walimu wakuu wawili ndani ya wiki mbili kwa sababu kuna vyombo vya habari tuleteeni taarifa ya shule yoyote yenye michango isiyofuata utaratibu tutalala nao mbele”Alisema Waziri Ummy.

Waziri Ummy alisema Rais Samia ameendeleza elimu bila malipo sera iliyoanzishwa na Hayati Dkt John Magufuli ambaye alikuwa anatoa bilioni 23 kila mwezi na Rais Samia ameongeza Bilioni 26 kila mwezi kwa ajili ya kugharamia uendeshaji shule.

“Hivyo anapokuja mtoto wa shule za awali anapokuja kuandikishwa… mtoto wa darasa la kwanza mzazi anaambiwa atoe elfu 50,000, au 100,000 hatukubali DC usisite kumchukulia hatua mwalimu mkuu yoyote tunataka kuondoa vikwazo visivyo vya lazima kwa watoto wa Tanzania kupata elimu”Alisema

Waziri huyo alisema nafasi ya ukuu wa shule inaendana na posho hivyo kama wewe unajidai ni kiburi hutaki kuzingatia maelekezo ya serikali hautufai kuendelea kuwa kwenye ukuu wa shule.

Hata hivyo aliwapongeza Halamshauri ya Jiji Tanga kwa kuamua kubuni na kuanzisha ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ambayo itasaidia watoto wanaotoka maeneo ya kata ya Maweni.

“Katika hili niwapongeze Halmashauri ya Jiji la Tanga badala ya kwenda kurundika madarasa hayo sehemu moja ambayo haina nafasi mkaona ni bora kuondoa sehemu madarasa hayo na kuyapeleka sehemu nyengine ili kujenga shule sekondari mpya niwapongeza kwa sababu Jiji la Tanga tumepata madarasa 54 ya Rais Samia tunamshukuru sana”Alisema

Hata hivyo aliwaongeza Halmashauri ya Jiji hilo kwa kutumia mapato ya ndani kujenga matundo ya vyoo 12 ikiwemo kuanza kujenga maabara moja huku akilazimika kutoa agizo hilo kwa nchi nzima.

“Rais Samia Suluhu ametuwezesha tumejenga madarasa ya sekondari 12000 ya shule shikizi 3000 nchi nzima hivyo niwaagize wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kutumia mapato ya ndani kujenga matundu ya vyoo kwa ajili ya wanafunzi”Alisema

Awali akizungumza Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa alisema wana Tanga wataendelea kumuomba dua Rais Samia Suluhu kutokana na juhudi kubwa za kimaendeleo anazowapelekea watanzania.

Alisema kwamba sambamba na mradi huo ambao ulikuwa nyuma kupita miradi yote kutokana na kwamba hiyo ni shule mpya kutokana na kwamba walikuwa hawana eneo wakatafuta walipopata wakaanza kusafisha na kuanza ujenzi wake.

Alisema shule zao nyengine wamekwisha kuzikamilisha kwa asilimia 100 na madarasa tayari 200 wamekwisha kamilisha ikiwemo kumalizia madawati 500 yaliyokuwa yamebaki na zoezi lililopo ni kuunganisha.

Alisema kwenye ujenzi huo kuna salio la fedha ambalo litakuwa limebaki kuweza kutekeleza miradi mingi na amemuomba Waziri Ummy na Baraza la madiwani kwamba ikiwezekana shule hiyo iwe maalumu kwa ajili ya wasichana ili waweze kuendelea kutoa hamasa kwao hata ikiwezekana iitwa jina lako.

Awali akizungumza katika ziara Mwalimu Mpokigwe Anyatike wa shule ya Sekondari Maweni ambaye pia ni Msimamizi wa mradi huo alisema mradi huo ujenzi huo ulianza Novemba 8 mwaka jana chini ya mpango wa madarasa ya Uviko 19 yenye thamani ya Milioni 280.

Alisema mradi huo wa ujenzi wa shule hiyo ulikuwa na dhamira ya kupunguza msongamano madarasani pia kuwapunguzia umbali wanafunzi wanaosishi mbali na maeneo ya shule ya sekondari maweni.

Alisema pamoja na madarasa 14 na ofisi mbili za walimu chini ya mpango za Uviko 19 halmashaueri iliamua kujenga choo na maabara kupitia mapato ya ndani ambapo sh milioni 20 za awali ziliingizwa na baadae milioni 50 ziliingizwa kwa ajili ya kumalizia ujenzi huo wa maabara na vyoo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.