Habari za Punde

Maadhimisho ya Siku ya Lugha Mama Duniani.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) Dkt.Mwanahija Ali Juma, akielezea jinsi Maadhimisho ya siku ya Kiswahili na Mashindano ya Insha yatavokuwa, ikiwa ni siku ya lugha Mama Duniani, huko Ukumbi wa TC Kiembe Samaki Mjini Zanzibar.

Na Pili Ali.  HABARI MAELEZO. 21/02/2022.

Imeelezwa kuwa ipo haja ya kuithamini na kuitunza lahaja katika jamii kwani ina nafasi  kubwa katika kuleta maendeleo.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) Dkt Saade Said  Mbarouk wakati akifungua kikao cha ufunguzi wa maadhimisho ya Siku ya Lugha  Mama Duniani yaliyofanyika katika Ukumbi wa TC Kiembe samaki mjini Zanzibar.

Amesema , bila ya kuwa na lugha mama katika jamii kuna uwezekano mkubwa wa kutokuwa na maendeleo kwani lugha ndiyo kiungo cha mawasiliano ambacho humuunganisha mtu au jamii katika kufanikisha mambo mbalimbali.

Aidha amewataka wanafunzi waliohudhuria katika maadhimisho hayo kwenda kuwashajihisha na wenzao  kuwa na utamaduni wa kuandika makala za Kiswahili ili  kuimarisha lugha mama katika jamii.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar ( BAKIZA)  Mwanahija Ali Juma amesema kuwa matumizi ya lahaja yanaweza kutumiwa na watu wa Jamii  tofauti ili isipotoshwe  na kwenda kinyume na maana iliyokusudiwa na kupoteza uhalisia wake.

Pia ametoa wito kwa kila jamii kuhakikisha inazungumza lahaja na kwafundisha watoto wao katika makuzi yao ili isiweze kupotea.

Vile vile amesisitiza maneno ya Rais wa awamu ya kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar marehemu mzee Abeid Amani Karume ya kwamba maofisi yote itumike lugha ya Kiswahili ambayo ni lugha kuu ya Taifa la Tanzania.

Nae mwalimu wa somo la lugha ya Kiswahili Skuli ya Sekondari ya Kiponda, Bi Maryam Khamis Mbarouk akitoa mchango wake juu ya mada ilyotolea amesema  iwapo lugha itakosa watumiaji kuna uwezekano mkubwa wa kupotea au kufa kabisa.

Hivyo ameiomba jamii kudumisha Utamaduni wa kutumia lahaja zao ili kutunza na kuimarisha zaidi lugha mama katika jamii zetu.

Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) Dkt. Saade Said Mbarouk, akifungua Kikao cha siku ya lugha Mama Duniani, kilichofanyika Ukumbi wa TC Kiembe Samaki Mjini Zanzibar.
Mratibu wa Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) Amour Salim Said, akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa Lugha Mama , ikiwa ni siku ya lugha Mama Duniani, huko Ukumbi wa TC Kiembe Samaki Mjini Zanzibar.
Mwalimu kutoka Skuli ya Kiponda Maryam Khamis Masoud, akichangia mada inayosema umuhimu wa Lugha Mama , ikiwa ni siku ya lugha Mama Duniani, huko Ukumbi wa TC Kiembe Samaki Mjini Zanzibar.
Baadhi ya Washiriki waliyohudhuria katika  siku ya lugha Mama Duniani, wakiwemo Wanafunzi na Walimu wa Kiswahili, huko Ukumbi wa TC Kiembe Samaki Mjini Zanzibar.
Baadhi ya Washiriki waliyohudhuria katika  siku ya lugha Mama Duniani, wakiwemo Wanafunzi na Walimu wa Kiswahili, huko Ukumbi wa TC Kiembe Samaki Mjini Zanzibar.
Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) Dkt. Saade Said Mbarouk, akifungua Kikao cha siku ya lugha Mama Duniani, kilichofanyika Ukumbi wa TC Kiembe Samaki Mjini Zanzibar.
(PICHA NA MARYAM KIDIKO - MAELEZO ZANZIBAR)


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.