Habari za Punde

Mkutano wa 6 wa Baraza la Kumi la Wawakilishi Zanzibar Kuaza Febuari 16 ,2022.

Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali Zanzibar wakimsikiliza Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Bi.Raya Issa Mselem, wakati akitowa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu shughuli za mkutano wa Sita wa Baraza la kumi la Wawakilishi Zanzibar unaotarajiwa kuanza febuari 16 ,2022.

Katibu wa Baraza la Wawakilishi Raya Issa Mselem Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu shughuli za mkutano wa sita wa Baraza la kumi la Wawakilishi zinazotarajiwa kuanza febuari 16 ,2022.

Picha na Fauzia Mussa -Maelezo Zanzibar.

Na Mwashungi Tahir       Maelezo Zanzibar- 14-02-2022.

Mkutano wa sita wa Baraza la kumi la Wawakilishi Zanzibar unatarajiwa kuanza siku ya Jumatano, Febuari 16 , 2022  saa tatu za asubuhi huko Chukwani Zanzibar.

Katibu wa Baraza la Wawakilishi Raya Issa Mselemu ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi kuhusuu shughuli za mkutano huo.

Akielezea shughuli za mkutano  huo amesema Afisi ya Baraza la Wawakilishi imepokea na kuratibu masuala 158 kwa ajili ya mkutano huo.

Aidha Katibu huyo ameseme kutakuwa na uwasilishwaji wa Ripoti za kamati za kudumu za Baraza hilo kwa mwaka 2020/2021.

Katibu Raya amesema mswaada mmoja utaletwa kwa hati ya dharura ambao mswada wa sheria ya kurekebisha sheria ya udhibiti wa fedha haramu na mapato yatokanayo na uhalifu Nam .10 ya 2009.

Aidha miswaada miwili ya sheria itasomwa kwa mara ya kwanza ambayo ni mswada wa Sheria ya kuanzisha Taasisi ya uhasibu ,wakaguzi na washauri elekezi wa wa Kodi Zanzibar na Mswada mwengine ni Sheria ya kuanzisha wakala wa uwezeshaji wananchi kiuchumi Zanzibar .

Katibu Raya amesema kutakuwa na taarifa ya Serikali juu ya Hali ya Utekelezaji wa miradi inayotokana na fedha za IMF za UVIKO 19 , Zanzibar .

Katibu huyo aliongeza kuwa katika Mkutano wa Baraza hilo kutakuwa na taarifa ya Wabunge watano  wanaoliwakilisha Baraza katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.