Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Aongoza Wananchi Katika Kuuaga Mwili wa Dr.Mwelecela Ntuli Malecela Viwanja Vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Hussein Ali Mwinyi akitia saini kitabu cha maombolezo  katika msiba wa  Mtoto wa Mzee John Samuel Malecela  Dr.Mwelecele  Ntuli  Malecela aliyekuwa mfanyakazi wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Majaliwa Kassim Majaliwa mara alipowasili  katika msiba wa  Mtoto wa Mzee John Samuel Malecela  Dr.Mwelecele  Ntuli  Malecela aliyekuwa mfanyakazi wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Hussein Ali Mwinyi akitoa salamu zake na kutoa pole kwa familia ya  Mzee John Samuel Malecela kwa kufiliwa na mtoto wake  Dr.Mwelecele  Ntuli  Malecela  aliyekuwa mfanyakazi wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) hafla iliyofanyika leo katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu  Mzee John Samuel Malecela (katikati) akiwa na familia yake katika msiba wa kumuaga Mtoto wake marehemu Dr.Mwelecele  Ntuli  Malecela  aliyekuwa mfanyakazi wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) hafla iliyofanyika leo katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wananchi mbali mbali waliohudhuria katika hafla ua kuuaga mwili wa marehemu Dr.Mwelecele  Ntuli  Malecela  aliyekuwa mfanyakazi wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) hafla iliyofanyika leo katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Hussein Ali Mwinyi akitoa salamu zake za mwisho na kuuaga  mwili wa marehemu Dr.Mwelecele  Ntuli  Malecela aliyekuwa mfanyakazi wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) Mtoto wa Mzee John Samuel malecela  leo katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Hussein Ali Mwinyi akitoa salamu zake za mwisho na kuuaga  mwili wa marehemu Dr.Mwelecele  Ntuli  Malecela aliyekuwa mfanyakazi wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) Mtoto wa Mzee John Samuel malecela  leo katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam leo.[Picha na Ikulu] 19/02/2022.













Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Hayati Dr, Mwelecele  Ntuli Malecela (Dr. Mwele) ni mwanataaluma aliejitolea kwa dhati kulipigania Taifa la Tanzania, ili kufikia lengo la kuondokana na magonjwa yasiopewa kipaumbele.

Dk. Mwinyi amesema hayo katika salamu alizotoa kwa waombolezaji wakati wa kuaga mwili wa Hayati Dr. Mwelecele Ntuli Malecela, hafla iliofanyika katika viwanja vya Karimjeee Jijini Dar es Salaam.

Amesema katika kipindi cha miaka 30 akiwa mtumishi wa Serikali katika taasisi ya Utafiti wa magonjwa  yasiopewa kipaumbe(NIMRY), Hayati Dr. Mwele alifanya kazi kubwa ya kuanisha Programu ili kutokomeza magonjwa yasiopewa kipaumbele, ikiwemo Matende na mabusha, minyooo ya Tumbo, kichocho, Trachoma pamoja na Usubi.

 

Alisema Hayati Dr. Mwele alifanya kazi kubwa ya kulitumikia Taifa , hivyo akawataka Watanzania kujitathmin  endapo  utumishi wao utafikia kiwango kilichoachwa na hayti Dr. Mwele.

 

Akizungumza kwa niaba yake na kwa niaba ya Familia ya Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mwinyi amesema kifo cha Hayati Dr. Mwele kimemgusa kila Mtanzania, kwani alikuwa mtu wa watu alietumia muda wake wote kuwatumikia wananchi.

 

Akinukuu kauli za viongozi wa Dini, aliwataka Watanzania kujifunza kutoka kwa yale yaliofanywa na Dk. Mwele, kwa kutambua kuwa  kutokana na vifo hupatikana mawaidha pamoja na hadithi njema.

 

Aidha, alisema ni wajibu wa wananchi kumuombea Dua hayati Dr. Mwele, pamoja na kuiombea familia yake ustahamilivu katika kipindi hiki kigumu.

 

Nae, Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa katika salamu zake alisema kifo cha Hayati Dr. Mwele kimeleta huzuni kubwa kwa kuzingatia mchango wake mkubwa aliotoa katika kulitumikia taifa.

 

Aidha, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Akson aliwataka Watanzania kuendeleza mambo mema yalioachwa na hayati Dr. Mwele, kwa maslahi ya Taifa na watu wake, huku akiwatakia pole wafiwa.

 

Katika hatua nyengine, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Joseiph Sinde Warioba alisema Hayati Dr. Mwele alikuwa mwanamke anaejiamini sana, kiasi ambacho katika mwaka 1995 alifikia uamuzi wa kuchukua fomu kugombea kiti cha Urais.

 

Dr. Mwelecele Ntuli Malecela aliekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) anaeshughulikia magonjwa yasiopewa kipaumbele alizaliwa mnamo mwaka 1963 na kufariki dunia mapema wiki Geneva Switzerland, wakati akiwa nchini alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu nchini Tanzania (NIMR).   

 Imetayarishwa na Kitengo cha Habari,

Ikulu Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.