MKUU wa Wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib
Yahaya, akizoa taka na kutia katika bero wakati wa zoezi la usafishaji wa Fukwe
ya Vumawimbi, iliyopo kijiji cha Makangale Wilaya ya Micheweni ikiwa utangazaji
wa Ufukwe huo kwa watalii.(PICHA NA ABDI
SULEIMAN, PEMBA)
WATENDAJI wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Rashid Abdalla Rashid na Mkurugenzi wa
Baraza la Mji Wete Salma Abouu Hamad, wakifagia ufukwe wa Vumawimbi ikiwa ni
ishara ya zoezi la ufanyaji usafi katika fukwe hiyo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba na Kaimu Mkuu wa
Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mattar Zahor Masoud (kushoto) akifukiwa takataka
katika moja ya shimo walilolichimba, wakati wa zoezi la ufanyaji usafi ufukwe
wa Vumawimbi, katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Abdalla Rashid Ali na
Mkuu wa Wilaya ya Wete Mgeni Khatib Yahara.(PICHA
NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MKUU wa Wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya
akimimina taka katika bero kwa ajili ya kwenda kutupwa sehemu maalumu, wakati
wa zoezi la ufanyaji usafi katika Fukwe ya Vumawimbi Wilaya ya Micheweni.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba na Kaimu Mkuu wa
Mkoa wa Kaskazini Pemba Matar Zahor Masoud, (katikati) akiwaongoza viongozi
mbali mbali wa serikali katika kusafisha ufukwe wa Vumawimbi Wilaya ya
Micheweni, ikiwa ni Zoezi la Kufanya usafi katika fukwe hiyo iliyoko Micheweni.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
No comments:
Post a Comment