Habari za Punde

Kikao cha kujadili masuala ya Ardhi na namna ya kutatua migogoro

MRATIB Kamisheni ya Ardhi Said Saleh Makame, akizungumza kikao cha kujadili masuala ya Ardhi na namna ya kutatua migogoro na kuwashirikisha Masheha na baadhi ya wananchi wa Micheweni, kikao kilichofanyika ukumbi wa halmashauri ya Micheweni.

MKUU wa Wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya, akifungua kikao cha kujadili masuala ya Ardhi na namna ya kutatua migogoro kilichowashirikisha Mashena na baadhi ya wananchi wa Micheweni, kikao kilichofanyika ukumbi wa halmashauri ya Micheweni.

NAIBU Mrajis wa Ardhi Pemba Asha Suleiman Said, akiwasilisha mada juu ya sheria na taratibu za ardhi katika utatuzi wa migogoro, mkutano uliowashirikisha masheha na baadhi ya wananchi wa Micheweni, kikao kilichofanyika ukumbi wa halmashauri ya Micheweni.

BAADHI ya washiriki wa mkutano wa kujadili masuala ya Ardhi na namna ya kutatua migogoro, mkutano ulioandalia na kamisheni ya Ardhi Pemba na kufanyika ukumbi wa halmashauri ya Micheweni.

AFISA Usajili wa Ardhi Pemba Yussuf Hamad Kombo, akiwasilisha mada Taratibu za utambuzi na usajili wa Ardhi, mkutano uliowashirikisha masheha na baadhi ya wananchi wa Micheweni, kikao kilichofanyika ukumbi wa halmashauri ya Micheweni.

(PICHA NA ABDI SULEIMAN.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.