Habari za Punde

KONGAMANO LA KITAIFA LA WANAWAKE

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akizindua tafiti ya matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto uliofanyika na Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru katika kupambana na vitendo hivyo katika jamii.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akizindua Programu ya mafunzo kwa Wasichana na daftari la kieletroniki la wajasiriamali na matokeo ya uzinduzi huu ni kuwawezesha wasichana kupata mafunzo ya Uongozi na kuwawezesha wajasirimali Machinga kwa kuwatambua na kuwasajili kwa lengo la kuwaunganisha katika fursa mbalimbali.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la UN Women Hoddan Addou na Balozi wa Ireland nchini Mhe. Mary Oniel mara baada ya Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililofanyika mkoani Arusha.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akitia saini katika kibango mara baada ya kuzindua Programu ya mafunzo kwa Wasichana na daftari la kieletroniki la wajasiriamali na matokeo ya uzinduzi huu ni kuwawezesha wasichana kupata mafunzo ya Uongozi na kuwawezesha wajasirimali Machinga kwa kuwatambua na kuwasajili kwa lengo la kuwaunganisha katika fursa mbalimbali
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akizungumza katika Kongamano la Kitaifa la Wanawake linalofanyika mkoani Arusha.

 Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika Kongamano la Kitaifa la Wanawake linalofanyika mkoani Arusha kwa lengo la kuwakutanisha Wanawake katika masuala mbalimbali yahusuyo maendeleo ya Wanawake na taifa kwa ujumla.

 

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WMJJWM



Na WMJJWM Arusha

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju ameiasa jamii kupambana na vitendo vya ukatili hasa dhidi ya Wanawake ili kutorudisha nyuma juhudi za Serikali na wadau za kuleta Usawa wa kijinsia.

 

Ameyasema hayo mkoani Arusha katika Kongamano la Kitaifa la Wanawake lililowakutanisha Wanawake na wadau wengine kujadili changamoto zinazowakabili Wanawake na Ustawi wao.

 

Ameongeza kuwa jamii inatakiwa kusimama katika kupambana na kupinga Mila hasi za kumnyima mwanamke haki na kumkandamiza katika kupata fursa mbalimbali zinazojitokeza kwenye jamii ili kumuwezesha mwanamke kuwa na uwezo wa kutatua changamoto zinazomkabili.

 

Aidha ameitaka Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru kusaidia kubadili fikra kwenye jamii ya namna wanavyomthamini na kumshirikisha mwanamke katika masuala mbalimbali hasa yanayohusu maamuzi ndani ya familia na jamii.

 

Pia ameitaka jamii na wadau mbalimbali kuendelea kutoa taarifa ya vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto katika vyombo husika ili kusaidia juhudi za Serikali na wadau kupambana na vitendo vya ukatili ili kuwa na Tanzania isiyo na vitendo vya ukatili.

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya uendeshaji Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt. Rosemarie Mwaipopo amesema Taasisi itaendelea kusimamia utekelezaji wa afua mbalimbali za kuhakikisha wanawake wanawezeshwa ili kuhakikisha wanapata fursa sawa katika Sekta mbalimbali.

 

Naye Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt Bakari George amesema lengo la Kongamano hilo ni kuwakutisha Wanawake na Makundi mengine na kuhakikisha kuwa Wanawake wanapata fursa mbalimbali zikiwemo za kiuchumi

 

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashirika Peter Mathuki amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha Usawa wa kijinsia unazingatiwa katika kipindi chake cha uongozi hasa mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto hivyo ameihakikishia Wizara kuendelea kushirikiana nayo ili kuunga mkono mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili.

 

Akizungumza katika Kongamano hilo Mkurugenzi wa Shirika la Legal Service Facility (LSF) Lulu Ng'wanakilala amesema Shirika lake litaendelea kusaidia Wanawake kupata haki zao katika masuala ya kisheria na kusema kuwa kati ya matukio kumi matukio manne yanayoripotiwa katika takwimu za Shirika hilo matukio hayo ni ya unyanyasaji wa Kijinsia ikiwa ni sawa na asilimia 26.4.

 

Katika hatua nyingine Naibu Katibu Mkuu Amon Mpanju amezindua Programu ya mafunzo kwa Wasichana na daftari la kieletroniki la wajasiriamali na matokeo ya uzinduzi huu ni kuwawezesha wasichana kupata mafunzo ya Uongozi na kuwawezesha wajasirimali Machinga kwa kuwatambua na kuwasajili kwa lengo la kuwaunganisha katika fursa mbalimbali.

 

Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Shirika la Legal Service Facility (LSF) imeandaa Kongamano la Kitaifa la Wanawake lenye lengo la kuwakutanisha Wanawake na wadau wengine katika kujadili changamoto zinazowakabili Wanawake na Ustawi wao.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.