Habari za Punde

CCM Yawataka Wateule wa Rais Kuelezea Mafanikio ya Serikali.

 

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Ndg. Shaka Hamdu Shaka akizungumza na Wanachama wa CCM NA Viongozi wa ngazi mbalimbali wakati wa ziara yake Mkoani Manyara. 

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimetoa maelekezo kwa wateule wa Rais Samia Suluhu Hassan wakiwemo wakurugenzi,wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kuelezea mafanikio yaliyopatikana katika Serikali ya Awamu ya Sita.

Kimesema kinashangazwa na ukimya uiopo kwa viongozi wa ngazi mbalimbali kushindwa kuelezea mafanikio lukuki ambayo yamekuwa yakifanyika katika maeneo yote nchini hali iliyoelezwa ni kutomtendea haki Rais Samia ambaye ameendelea kutoa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Akizungumza mbele ya viongozi na Wana-CCM Mkoa wa Manyara leo Mei 14, 2022 ,Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho shaka Shamdu Shaka ametumia kikao hicho kuelezea kuwa tangu Rais Samia aingie madarakani amefanya kazi kubwa na nzuri ya kuwatumikia wananchi ikiwa pamoja na kupeleka maendeleo lakini cha kushangaza hakuna anayesema, wamekaa kimya.

“Tunayo kazi wana CCM kuunga mkono juhudi hizi ambazo viongozi wetu wakiongozwa na Rais Samia ambaye ni Mwenyekiti wetu Taifa, kazi kubwa inafanyika na bahati mbaya sana Serikali ya CCM inatoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu lakini bado kumekuwa na ukimya wa kusema juhudi hizi zinazofanywa na Serikali, kila mmoja anayo dhamana ya kuisema serikali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.